Maswali kumi sumu mwilini mwa Mangula
NancyTheDreamtz
KAULI
ya Jeshi la Polisi kwamba Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula alipewa sumu, imeacha maswali mengi
na mjadala mkubwa miongoni mwa jamii.
Februari 28, mwaka huu, Mangula alidondoka ghafla
katika ofisi ndogo za CCM Lumumba mara baada ya kumaliza kikao cha
Kamati Kuu ya CCM kilichokuwa kikijadili masuala mbalimbali, ikiwamo
adhabu kwa wanachama watatu waliokuwa na tuhuma za ukiukwaji wa maadili
ndani ya chama hicho.
Katika kikao hicho,
aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, alivuliwa uanachama kwa
tuhuma za ukiukwaji wa maadili kwa mujibu wa katiba ya chama hicho na
kanuni ya maadili na uongozi.
Tuhuma hizo pia
zilikuwa zikiwakabili makatibu wakuu wastaafu wa chama hicho,
Abdulrahman Kinana ambaye atakuwa chini ya uangalizi kwa miezi 18 na
Yusuf Makamba aliyesamehewa makosa yake.
Akizungumza
jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro
Mambosasa, alisema kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na
usalama, wamebaini ndani ya mwili wa Mangula kulipatikana sumu.
“Machi
2 tulipokea taarifa kutoka uongozi wa CCM kuhusu kuwekewa sumu Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara, Mangula. Katika taarifa hiyo tulielezwa kwamba
Mangula alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kulazwa chumba cha
uangalizi maalumu (ICU).
“Uchunguzi kuhusu
tuhuma ya sumu hiyo ilivyoingia mwilini upelelezi bado unaendelea. Jeshi
la Polisi litachukua hatua kali kwa mtu yeyote atakayebainika kupanga,
kuratibu au kusimamia utekelezaji wa uhalifu huo.
“Haitajalisha
awe ni mwanafamilia, awe ni mtu kutoka ndani ya CCM au vyama vingine
vya siasa, mwananchi wa kawaida, awe ndani au nje ya nchi, awe
serikalini au taasisi yoyote hatua kali zitachukuliwa,” alisema
Mambosasa.
Aliwataka wananchi wajiepushe na vitendo hivyo kwani si tu vya kinyama, bali pia vinalenga kukiuka sheria za nchi.
MASWALI KUMI TATA
Kutokana
na uzito wa tukio hilo bado limezua sintofahamu katika jamii, huku
kukiibuka maswali ambayo hadi sasa bado yamekosa majibu na kusubiri
taarifa ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi.
Baadhi ya maswali hayo ambayo jamii inahitaji kujua majibu yake ni kwamba Mangula alikuwa wapi baada ya kutoka nyumbani kwake.
Je,
aliamkia wapi? Kifungua kimya gani alipata? Usafiri gani alitumia kwa
siku hiyo kabla ya kuanguka? Je, alisalimiana na nani? Je, ofisini
aliingia saa ngapi na alikutana na nani? Je ni nani alimuhudumia kupata
kifungua kinywa ? Je wakati wa kikao alikula na kunywa? Je,
alihudumiwaje? Na mfumo wa huduma ulikuwaje?
Pamoja na hayo bado Watanzania wanasubiri na kutaka kujua maendeleo ya afya yake.
JPM ALIVYOMJULIA HALI
Februari
29, mwaka huu, Rais Dk. John Magufuli alimtembelea na kumjulia hali
Mangula ambaye alikuwa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Rais, Ikulu, Gerson
Msingwa, Mangula aliugua ghafla na kisha kukimbizwa hospitali kwa
matibabu.
Kwa mujibu wa video za Ikulu, Magufuli alionekana akimwombea Mangula kupona kwa haraka.
“Utapona
na Mungu atakusimamia utarejea katika majukumu yako, nilikuona jana
(Februari 28) umeanguka, ilitushtua,” alisema Rais Magufuli huku
Mangula akisema “sijui niliangukaje.”
Hata
hivyo Rais Magufuli, alisema kuwa hawezi kujua kwani wanamkabidhi Mungu
ambaye atamsimamia siku zote kwa sababu wanadamu wanalindwa na Mungu
ambaye huwapenda sana.
Rais Magufuli alimwomba Mangula kufanya ibada hospitalini hapo na alifanya hivyo.
VIONGOZI NA SUMU
Novemba
12, 2019 Rais Magufuli alisema wakati akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi
katika Serikali ya awamu ya tatu, alinyweshwa sumu kutokana na utendaji
wake wa kazi.
Alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Rais mstaafu Benjamin Mkapa kilichoelezea maisha yake.
“Tulipofanya
kazi vizuri kwenye kujenga barabara, mzee Mkapa alifurahi sana,
akatamka kwamba mimi ni askari wake wa mwavuli namba moja, ameligusia
hili kwenye ukurasa wa 107 wa kitabu chake.
Comments