Floyd Mayweather ‘MONEY’ kuinunua Newcastle United

NancyTheDreamtz

Mwanamasumbwi machachari raia wa Marekani, Floyd Mayweather a.k.a ‘Money’ ameonyesha nia yake ya kutaka kuinunua klabu ya Newcastle United inayoshiriki Premier League.
Image result for Floyd Mayweather interested in buying Newcastle
Bingwa huyo wa dunia, ‘Money’ ameongea hayo wikiend hii iliyopita akiwa kwenye sherehe nyakati za jioni kwenye ‘tour’ yake huko 02 City Hall.

Mashabiki wa Newcastle United wamekuwa wakimtaka mmiliki wa klabu hiyo ya England, Bilionea  Mike Ashley kuiuza baada ya uongozi wake wa miaka 13 pasipo mafanikio yoyote.

‘Money’ ni bondia mwenye mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja, anaaminika kuwa miongoni mwa wanamichezo wanao miliki mkwanja mrefu zaidi.

Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 43, katika mapambano 50 aliyopigana ameshinda yote, haja poteza hata moja. Inakumbukwa aliwahi kupigana na nyota wa UFC, Conor McGregor, amewahi pia kupambana na Oscar De La Hoya, Ricky Hatton, Manny Pacquiao na Canelo Alvarez ndani ya miaka yake 20 ya tasnia hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele