Jinsi Mgonjwa wa Kwanza wa CORONA Alivyoingia Uganda
NancyTheDreamtz Waziri wa Afya wa Uganda, Ruth Jane Aceng alisema kisa hicho kilichothibitishwa ni raia wa Uganda mwenye miaka 36 ambaye aliingia nchini humo akitokea Dubai Jumamosi Machi 21 saa 2 asubuhi kwa ndege ya Shirika la Ethiopia (Ethiopian Airlines). Dk Aceng alisema mtu huyo ni mkazi wa eneo la Kibuli Kangungulu katika mji mkuu Kampala. "Mtu huyo alisafiri kwenda Dubai Machi 17, kwa sababu za biashara. Wakati wa kusafiri kwake alikuwa mzima kiafya," alisema Dk Aceng. Aceng alisema mtu huyo kwasasa ametengwa katika Hospitali ya daraja la Entebbe. Abiria wote waliosafiri na mtu huyo wako chini ya uangalizi na hati zao za kusafiria zimeshikiliwa na Serikali. Siku ya Jumamosi, Rais Yoweri Museveni alitangaza kwamba Uganda imefunga mipaka yote ili kuzuia watu kuvuka nchini kwa lengo la kujilinda na ugonjwa huo ambalo limekuwa janga duniani baada ya kuripotiwa vifo zaidi ya 10,000. Museveni leo Machi 22, 2020 atazungumza kuhusu hatua zitak...