Skip to main content

Trump Akataa Kupima Corona ilihali waziri awekwa karantini


×

Trump Agoma Kupima Corona, Waziri Mkuu Awekwa Karantini

WAZIRI Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, na mke wake watabaki kwenye karantini kwa siku 14, baada ya mkewe, Sophie Gregoire Trudeau, kukutwa na virusi vya Corona na ambaye kwa mujibu wa mkurugenzi wa mawasiliano wa Waziri Mkuu,”anaendelea vizuri na dalili alizonazo si mbaya.”

Bwana Trudeau pia atakuwa kwenye karantini kama hatua ya tahadhari. Hatapimwa katika hatua za sasa kwa kuwa haonyeshi dalili za maambukizi. Katika ukurasa wa Twitter, Bi Sophie aliandika ”nitarejea nikiwa na afya njema hivi karibuni.”

Bi Trudeau amesema alikuwa amepata dalili ambazo hazikuwa za kawaida na kuongeza kuwa ”kuwa kwenye karantini si kitu ukilinganisha na familia nyingine nchini Canada wanaopitia haya. Ninawatia moyo na kuwaweka kwenye fikra zangu, ‘nawatakia afya njema.”

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema hana mpango wowote wa kupima virusi ingawa alikaribiana na afisa kutoka Brazil ambaye sasa amegundulika kuathirika na virusi hivyo. Ikulu ya Marekani imesema hakuwa na mazungumzo na afisa huyo wa Brazil, hivyo hakukuwa na umuhimu wa kupima.

Fabio Wajngarten, Waziri wa Mawasiliano wa Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro, aliweka kwenye mtandao wa Instagram picha yake akiwa amesimama karibu na Rais Trump. Makamu wa Rais, Mike Pence, pia alionekana kwenye picha.

Nchini Brazil
Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro, amechukuliwa vipimo na sasa anasubiri majibu. Hatua hii imekuja baada ya mawasiliano aliyoyafanya na mkuu wake wa mawasiliano, ambaye amekutwa na virusi vya Corona baada ya kurejea akitokea kwenye ziara nchini Marekani alipokutana na Rais Donald Trump.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeutangaza mlipuko wa virusi vya Corona kuwa ni janga la kimataifa, huku mlipuko huo ukiendelea kusambaa kwa kasi katika mataifa mbalimbali duniani. Mkuu wa WHO, Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema kuwa idadi ya visa nje ya China vimeongezeka mara 13 kwa kipindi cha majuma mawili yaliyopita.

Amesema kuwa “ana hofu kubwa ” kutokana na “viwango vya maambukizi ” ya virusi. Janga ni ugonjwa ambao unasambaa katika nchi nyingi kote duniani kwa wakati mmoja.

Nini kinachofanyika kwengine duniani?
Gavana wa New York ametangaza kuwa wanajeshi watapelekwa katika mji wa kaskazini wa New Rochelle, katika juhudi za kudhibiti mlipuko wa virusi huku visa vya maambikizi nchini Marekani vikipita 1,000 siku ya Jumatano.

Athari kubwa imeonekana nchini China. Lakini siku ya Jumapili iliripoti idadi ya chini zaidi ya maambukizi mapya katika siku moja tangu Januari,  ishara kwamba kuenea kwa virusi kunapungua. Iran, moja ya maeneo yenye maambukizi mabaya zaidi nje ya China, sasa imethibitisha maambukizi 6,566 na vifo 194.

Ufaransa, virusi vinaenea miongoni mwa wabunge. Wabunge wawili walikutwa na maambukizi, maafisa walieleza siku ya Jumapili. Kwa jumla manaibu maofisa wanne wameambukizwa. Pia Jumapili Ufaransa iliripoti visa 1,126, ongezeko la 19% kwa siku na idadi kubwa ya maambukizi barani Ulaya baada ya Italia.

Serikali ya Ufaransa imepiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya 1,000. Nchini Marekani, zaidi ya watu 470 wamekutwa na maambukizi ya Covid-19 na mpaka sasa waliopoteza maisha ni watu 21.

Miongoni mwa nchi zilizoripoti ongezeko la maambukizi ni Ujerumani 939, Uhispania 589, Uingereza 273 na Uholanzi 265. Albania, Bulgaria, Colombia, Costa Rica, visiwa vya Maldives, Malta, na Paraguay zimeripoti visa vya kwanza vya maambukizi ya virusi hivyo.



TOA COMMENT

Copyright 2019 Global Publishers | All Rights Reserved
Important message to the site owners. Do not ignore. Click here
Subscribe to notifications

Comments

Popular posts from this blog

Mbwana Misosi avurugwa: Unanivimbia wewe nani? mimi staa kabla yako, kama wewe sio shabiki yangu basi demu wako shabiki yangu (Video)