Harmonize Aanza Kupasua Anga Kumkalisha Diamond Platnumz Kupitia Afroeast

NancyTheDreamtz


 Wanapotajwa wasanii wakubwa wa Bongo Fleva nchi hii, jina la Harmonize haliwezi kuwekwa kando, licha ya kuingia katika tasnia hiyo miaka michache iliyopita.

Ni kama vile ameanza kupasua anga kivyake vyake nchi ya WCB, wiki iliyopita alidhihirishia hadhira kuwa ni miongoni mwa wasanii wakubwa wa muziki wa kizazi kipya, kwa kufanya uzinduzi wa kishindo wa albamu yake ya kwanza aliyoipa jina la Afroeast2020 yenye nyimbo 18 uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Harmonize anasema licha ya kutumia muda mwingi kubuni namna atakavyofanya uzinduzi huo, alichokuja nacho kilikubaliwa na wengi ikiwamo wasanii wenzake.

“Lakini nimejifunza kitu, kuwa napaswa niendelee kuwa mbunifu ili nieleweke na mashabiki wangu na wanaofuatilia muziki wa kizazi kipya.

“Muziki wenyewe kwa ujumla umekuwa sana, si ajabu kukuta wimbo wa Bongofleva unasikilizwa Marekani na kwingineko duniani, hivyo kuna kitu tunafanya kinachotakiwa kuongezwa vionjo zaidi,” alisema Harmonize.

Akinukuu maoni ya wasanii wenzake na viongozi alisema:


“Kama ambavyo alisema mama yetu Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson, siku ya uzinduzi wa albamu pale Mlimani City, kuwa tuongeze bidii zaidi tutafika mbali.

“Nami kama msanii nimeliona hilo na mawazo ya mashabiki, wasanii wenzangu yanaonyesha kuwa nimefanya kitu kikubwa, hivyo lazima niendelee kuwa mbunifu ili niendelee kufanya vitu vizuri zaidi,” alisema Harmonize.

Wasanii wengi wameonekana kuondoa makandokando yao na kukubali kazi ya msanii huyo ambayo aliwashirikisha wasanii wengi kutoka ndani na nje ya nchi.

Izzo Busness ni mmoja wa wasanii wakongwe hapa nchini, hakusita kuzungumzia albamu hiyo.

“Ukitizama jinsi kazi ilivyopangiliwa sio mchezo ni albamu iliyokwenda shule, mimi nampongeza sana dogo anaweza azidi kupambana zaidi,” alisema Izzo mtoto wa Mbeya.

Darassa

Ukitaja wasanii wanaofanya vizuri katika tasnia hiyo huwezi kumsahau Darassa, ambaye aliwahi kubamba na wimbo ‘Too Much’.

“Nyimbo zote 18 zilizomo ndani ya albamu hiyo kali, lakini kwangu mimi tano ndiyo zimenivutia zaidi.

“Nyimbo hizo ni ‘Konde Boy For Everybody’ ‘Afroeast2020’. Kwangu kali ni 14, 7, 12, 8 na 10 hizi nyimbo kali sana,” alisema Darassa.

Nyimbo alizozikubali Darassa ni namba 14 ni ‘Mama’ ambao umeonekana kukubalika na watu wengi , namba saba katika albamu hiyo ni ‘Never Give up’ aliomshirikisha The World namba 12 ni ‘Die’ aliomshirikisha Khali Graph na Dj Seven, namba nane ‘Wife’ aliomshirikisha Lady Jaydee huku namba 10 ukiwa ni ‘Malaika’ aliomshirikisha Morgan Heritage.

Comments

Popular posts from this blog

Mbwana Misosi avurugwa: Unanivimbia wewe nani? mimi staa kabla yako, kama wewe sio shabiki yangu basi demu wako shabiki yangu (Video)