PAUL Makonda Atamani Kigamboni Kufanana na Mji wa Manhattan Marekani

NancyTheDreamtz

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Jumanne Februari 11, 2020 amemuomba ruhusa Rais wa Tanzania, John Magufuli aweze kuifanya Wilaya ya Kigamboni kufanana na mji wa Manhattan uliopo Jiji la New York, Marekani.

Makonda ametoa kauli hiyo katika hafla ya uzinduzi wa jengo la manispaa ya Kigamboni na jengo la mkuu wa Wilaya hiyo eneo la Gezaulole Kigamboni.

"Niruhusu mheshimiwa Rais kupitia miradi ya maji, umeme, hospitali, barabara niifanye wilaya ya Kigamboni kuwa wilaya ya kisasa".

"Tumetembea huko duniani tumeona. Ukienda pale Manhattan, New York City upande wa pili utakuta kuna kisiwa cha Jersey, Kuna mambo mazuri. Haka ndio ka kisiwa ketu kawe na hoteli nzuri za kitalii, fukwe nzuri. Mtu akitaka kwenda kula maisha anasema ni Kigamboni hapana sehemu nyingine," amesema Makonda

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele