Mimi ni hazina kubwa, CCM watanilea na ipo tayari kuwaendeleza Watanzania na kule nilikotoka huo utayari siuoni” Dkt. Mashinji

NancyTheDreamtz


Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt Vicent Mashinji, leo Februari 18, 2020 amehamia Chama cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Hamphrey Polepole.


Dkt Vicent Mashinji, baada ya kupokelewa katika Ofisi ndogo za CCM, Lumumba

Akiwa katika ofisi ndogo za CCM Dkt Mashinji amesema kuwa baada ya kutafakari kwa muda juu ya mwenendo wa siasa nchini, aliona chama cha CHADEMA bado kiko mbali katika kuchochea suala zima la maendeleo ya vitu na watu.

“Malumbano ya Asubuhi mpaka Jioni nilikuwa naona yanatuchelewesha, nikaona ni heri nije hapa Lumumba, niongee na wenzangu nione kama nitapata fursa ya kutoa mchango kwenye Taifa langu, mimi bado ni kijana miaka 47 ninaweza nikawa hazina kubwa ambayo CCM kinaweza kikanilea na kunikuza zaidi” amesema Dkt Mashinji.



Usiku wa kuamkia Disemba 20, 2019 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, alimpendekeza Mbunge wa Kibamba John Mnyika kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho akichukua nafasi ya Dkt Mashinji.

"Ninaona kabisa Chama cha Mapinduzi kiko tayari kuendeleza Watanzania na kule niliko toka huu utayari siuoni" – Dkt. Mashinji – Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA 

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele