Posts

Showing posts from November, 2019

Vurugu Hotelini… Ebitoke Amponza Mlela! we

Image
NancyTheDreamtz KIKI imemtokea puani! Komediani na mwigizaji maarufu wa kike wa filamu za Kibongo asiyeishiwa vituko, Annastazia Exavery almaarufu kama Ebitoke, amempoza mwigizaji Yusuf Mlela, Amani limedokezwa. Jumatatu ya Novemba 11, mwaka huu, Ebitoke alivamia mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Mlela kwenye Hoteli ya Protea jijini Dar na kufanya vurugu zilizozua gumzo kila kona. TUKIO LA KUTENGENEZA (KIKI) Katika tukio hilo ambalo ni la kutengeneza (kiki) kwa asilimia mia moja, Ebitoke alifika mahali hapo na kwenda kumvua wigi mrembo aliyesemekana anatoka na Mlela aliyetajwa kwa jina la Beyonce na kumwacha akiwa na kipilipili kichwani, lakini lawama zote sasa zinaelekezwa kwa Mlela huku kukiwa na shinikizo la kuchukuliwa hatua. EBITOKE ALIA KUSALITIWA Kabla ya tukio hilo, siku chache zilizopita Ebitoke alilia mbele ya gazeti hili akilalamika kusalitiwa kimapenzi na kuchezewa na Mlela baada ya jamaa huyo kunaswa na Beyonce kwenye birthday ya mwigizaji Aunt Ezekie...

Fiesta Dar, Kwa mara ya kwanza kufanyikia Uwanja wa Taifa Alikiba Kutumbuiza

Image
NancyTheDreamtz Tamasha la Fiesta 2019 limefikia ukingoni na linatarajiwa kufanyika Desemba 8, 2019 Jijini Dar Es Salaam. Tamasha hilo kongwe kabisa la burudani Tanzania, Kwa mara ya kwanza litafanyika katika Uwanja wa Taifa hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waandaaji wa tamasha hilo Clouds Media. Kuhusu idadi ya wasanii watakaotumbuiza bado haijatajwa na mpaka sasa ni Alikiba pekee aliyethibitisha kuwa atatumbuiza huku orodha nyingine ndefu ya wasanii ikitarajiwa kutangazwa kuanzia leo kupitia vipindi mbalimbali vya Clouds FM.

Ruby Yamfika Hapa! Atoboa Mazito Anayoyapitia kutoka kwa Mzazi Mwenie "Nimepata Vipigo, Manyanyaso na Fedhea"

Image
NancyTheDreamtz Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kwenye ukurasa wa msanii Ruby, ameweka wazi visa ambavyo anafanyiwa na mpenzi wake aitwaye Kusah, kwa kupigwa,  kunyanyaswa, kudhalilishwa na kupewa kashfa za kujihusisha kwenye mahusiano na wasanii wa kiume. Hali inaashiria kwa sasa wawili hao wameachana na walibahatika kupata mtoto mmoja wa kike, ila Ruby aliandika kuwa yeye sio muongeaji sana wa mambo ila leo acha aongee. "Nimekuwa nikijiuliza niseme ama niongee kwa nani, huenda nayopitia au niliomaliza kupitia yanampata binti  wa kike mwenye umri kama wangu au zaidi yangu ila tu amekuwa kifungoni, Nimepitia vipigo, manyanyaso, fedhea, kudhalilishwa na kuitwa majina yote kutoka katika kinywa na mikono ya Mwanaume ambae alikuja kwangu kutaka support" ameandika Ruby. "Nimejitahidi kwa uwezo wangu kukuunganisha na kaka yangu, mwisho wa siku unishushie makofi natembea nae, ukuishia apo unayasambaza na ya mtu tunayeheshimiana Juma Jux kusema natembea naye, hi...

Utabiri wa Bongozozo mechi ya Stars,ataja mfungaji

Image
NancyTheDreamtz Shabiki wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' aliyejizolea umaarufu hivi sasa hapa nchini, Nicky, maarufu kama 'Bongozozo' ametoa utabiri wake kuelekea mchezo wa leo wa Taifa Stars dhidi ya Equitorial Guinea pamoja na mfungaji. Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa taifa, ikiwa ni kuwania kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika AFCON 2021 nchini Cameroon. Akizungumza na EATV & Radio Digital, Bongozozo amesema kuwa angependa Stars ishinde mabao manne au hata sita ili afurahi na kumtaja mshambuliaji Farid Mussa kuwa ndiye atakuwa mfungaji wa leo kwenye mchezo huo. "Ni muhimu sana uende uwanjani au usikilize na ufurahie mpira, ni kama sherehe fulani. Leo tutashinda magoli mengi tena itakuwa bila, inaweza kuwa tatu bila, mbili bila au ingekuwa sita bila ingekuwa balaa, lakini ninavyotabiri itakuwa mbili bila kwakuwa Kaseja hapitiki pale.", amesema Bongozozo. "Farid Mussa anafunga leo, nilienda kuonana naye nikampa ngucu za Bongoz...

Aussems: Hakuna wa kuzuia ubingwa Simba

NancyTheDreamtz K OCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, amefunguka kuwa ana uhakika mkubwa wa timu yake kuweza kutetea ubingwa wake msimu huu licha ya kupoteza mchezo uliopita kutokana na ubora wa kikosi chao. Simba bado inaongoza ligi ikiwa na pointi 18 kabla ya mchezo wa jana Jumapili dhidi ya Mbeya City na nyuma ya Kagera Sugar wenyewe pointi 16, wakati wapinzani wao wakubwa Azam wakiwa kwenye nafasi ya 13 wakiwa na pointi tisa huku Yanga wakiwa na pointi saba kwenye nafasi ya 17. Akizungumza na  Championi Jumatatu,  Aussems amefunguka kuwa bado wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa msimu huu na hakuna ambacho kitaweza kuwazuia kutokana na kasi ya wapinzani wao huku akiamini ubora wa timu yake kubadilika baada ya kufungwa na Mwadui wiki iliyopita. “Haikuwa mipango yetu kupoteza lakini wachezaji na benchi la ufundi tumegundua makosa yetu ambayo yamesababisha kutuondoa kwenye njia ingawa haijaweza kuharibu malengo ambayo tupo nayo kwenye ligi, maana u...

Diamond Platnumz Youngest Son’s Name Finally Revealed

Image
NancyTheDreamtz Diamond Platnumz youngest son’s name finally revealed Diamond Platnumz and his mum have finally gone ahead to reveal the name of the youngest Simba in their home. Judging from a post shared by Mama Dangote, we understand that Diamond Platnumz youngest son has been named after his daddy, Naseeb Junior. This comes as a big surprise since Hamisa Mobetto’s son had already been named after Diamond Platnumz but it appears that Mama Dangote was not satisfied by this hence the two Naseeb’s. Tanasha’s son So far many of their fans continue to wait for the 40 day celebrations that will be going down in a few days as promised by the WCB boss. Just like Latiffa Dangote, Naseeb Junior will be unveiled by his celebrity parents on his 40th day on earth and from the look of things people can’t wait to finally see him for the first time.

Yanga Yaanza na Straika Aliyeibeba Stars

Image
NancyTheDreamtz ZIKIWA zimebakia siku chache kabla ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili, uongozi wa Yanga tayari umeanza harakati zake za kukisuka upya kikosi chake kwa ajili ya kuhakikisha msimu huu timu hiyo inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara. Uongozi huo unaiangalia zaidi safu yake ya ushambuliaji ambayo tangu kuanza kwa msimu huu haijafanya vizuri kama mashabiki wengi wa timu hiyo walivyotarajia kutokana na utitiri wa washambuliaji wa kimataifa waliojiunga nayo mwanzoni mwa msimu huu. Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga ambazo Championi Jumatatu limezipata, zimedai kuwa uongozi huo hivi sasa upo katika mazungumzo na mshambuliaji wa kutumainiwa wa Azam FC anayeichezea Polisi Tanzania kwa mkopo. Mchezaji huyo si mwingine bali ni Ditram Nchimbi ambaye hivi karibuni alifanikiwa kuipiga Yanga hat trick katika mchezo wa ligi kuu kwenye Uwanja wa Uhuru. Lakini pia kama haitoshi, Nchimbi alifanya kweli alipokuwa na timu ya taifa ‘Taifa Stars’ huko nchini Sudan ambapo ali...