UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

NancyTheDreamtz
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC) leo Septemba 16, 2019, Imemuidhinisha mchezaji wa zamani wa Inter Milan na timu ya taifa ya Kenya, McDonald Mariga, kugombea ubunge katika jimbo la Kibra kwa tiketi ya Chama cha Jubilee.
McDonald Mariga aliyevaa kofia
Wiki iliyopita, uteuzi wa McDonald Mariga uliotangazwa na Chama cha Jubilee, uliingia dosari baada ya kukataliwa na Tume hiyo kwa madai kuwa taarifa zake zinakinzana.
Kwenye uchaguzi huo, Mariga atachuana na msanii maarufu wa muziki nchini humo, Prezzo ambaye anagombea ubunge kwa tiketi ya chama cha Wiper.
Mgombea mwingine ni Imran Okoth atasimama kwa tiketi ya Chama cha ODM, Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kibra utafanyika Novemba 7, mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele