Posts

Showing posts from August, 2019

Nicki Minaj Amuita Rick Ross Takataka Asema " Sitaki Kumsikia Mtu Anayemtukana Mwanamke Ili Auze Album Yake"

Image
NancyTheDreamtz Swali lililoulizwa na Joe lilionekana kumkwanza mwanadada Nicki Minaj baada ya kumuuliza kwamba ni nani mkali kati ya The Game na Rick Ross? Majibu ya Minaj yalikuwa makali zaidi kwa Rozzy baada ya kusema kuwa:- “Hebu usiniletee hapa hiyo takataka, usinifanye nianze kumuongelea. Mtu yeyote anayemtukana mtoto wa Kike ili kuuza vinakala 250 vya album, usimlete kabisa mbele yangu. Hongera kwa The Game, anajua kuchana.” alizungumza Nicki. Alienda mbali zaidi na kusema; Rozay hana fadhila kwa sababu alim-diss vibaya licha ya kuwahi kumsaidia msanii wake (Meek Mill) tena mbele ya Rais Obama kipindi wana mahusiano na alikuwa ameandamwa na matatizo ya kisheria. “Nilienda kukutana na Obama, na Ross alikuwepo. Nilienda kuongea naye kuhusu masuala ya “Probation” baada ya kikao nilimuona Rozay akimtumia meseji Meek na kumuambia ‘Huyu mwanamke ni wa kumtunza sana’ Halafu leo unakuja kutoa Ki-album chako na kunitukana mimi, kalisha makalio yako manene huko” Alisema Minaj

Amber Lulu 'Mimi sio wa Kufeki Maisha..Ni Kweli Nilikuwa Sina Kodi ya Nyumba Nandy Akaokoa Jahazi'

Image
NancyTheDreamtz BAADA ya habari kutapakaa kama moto wa kifuu akikiri kuokolewa na msanii mwenzake, Faustina Charles ‘Nandy’ baada ya kumlipa hela shoo na kulipa kodi, msanii wa Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ amewamaindi watu mitandaoni wanaomsema vibaya kuhusu hilo. Akizungumza na Za Motomoto ya Risasi, Amber Lulu alisema kuwa yeye siyo wa kufeki maisha hata siku moja na ni kweli alikuwa hana kodi na hela aliyompa ilimsitiri sana mbali na kulipia kodi. “Eti utakuta mtu anasema huna aibu kusema nilikuwa sina kodi kwa kumuogopa nani sasa na kwa nini maana amenipa kazi na nimefanya akanilipa shida iko wapi na nani anaumia sasa?” alimaindi Amber Lulu.

Kardinali Pengo Ang’atuka Rasmi, Papa Francis Aridhia

Image
NancyTheDreamtz ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp  Kardinali Pengo, ameng’atuka wadhifa huo na nafasi yake imechukuliwa na Askofu Mkuu Mwandamizi, Yuda Thaddeus Ruwa’ichi, wa Jimbo kuu la  Dar es Salaam. Hivi karibuni, Askofu Pengo aliomba kupumzika nafasi hiyo ambapo Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis ameridhia ombi hilo na kumruhusu kupumzika.

Kitumbo cha Tanasha Gumzo

Image
NancyTheDreamtz GUMZO kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ni muonekano mpya wa mpenzi wa mwanamuziki maarufu Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch baada ya kuingia studio kisha kupiga picha zikimuonesha na kitumbo chake.   Tanasha anatarajiwa kujifungua wakati wowote kuanzia sasa ambapo inaelezwa kuwa, sasa hivi ujauzito wake una miezi ipatayo nane na imembadili muonekano wake huku akipenda sana kulianika tumbo hilo. Akizungumza na Amani, rafiki wa karibu wa Diamond aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, mara ya mwisho kumuona laivu Tanasha alimshuhudia akiwa na tumbo kubwa na mara kwa mara alikuwa akijipiga picha za ukumbusho. “Mimi nimemuona, kwa kweli mimba imemkubali na vile anavyojipenda sasa ndiyo amezidi kuwa ‘mtamu’, lakini anaonekana kuwa na kaugonjwa ka’ kujipiga picha. Kila wakati atapozi na kukuomba umpige picha huku akiweka mapozi tofauti,” alisema mtoa habari huyo. Katika kudhihirisha kuwa Tanasha amekuwa na kaugonjwa ka’ picha, mwanadada...

“Tupeni Huo Ujanja Nyie Mnafanyaje Mmefanikiwa” Magufuli kwa Ramaphosa

Image
NancyTheDreamtz Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuomba Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Matamela Cyril Ramaphosa kuwahamasisha zaidi wafanyabiashara wa Afrika Kusini kuja kuwekeza hapa nchini kwa kuwa Tanzania inayo dhamira ya dhati ya kuongeza ushirikiano wake na nchi hiyo katika nyanja mbalimbali za kiuchumi. Rais Magufuli amesema katika kutekeleza mipango yake ya maendeleo na dira ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 Tanzania inawakaribisha wawekezaji mbalimbali, kwa kuwa Afrika Kusini imepiga hatua kubwa katika viwanda amewaalika wafanyabiashara wa nchi hiyo kuja kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo dawa na vifaa tiba, kuchakata madini na kwamba Serikali itatoa ushirikiano wowote utakaohitajika. Rais Magufuli pia amemuomba Rais Ramaphosa kuongeza ushirikiano na Tanzania katika utalii, hasa ikizingatiwa nchi hiyo inapokea watalii zaidi ya Milioni 10 kwa mwaka ikilinganishwa na Watalii Milioni 1.5 wanaoingia hapa n...

LIVE SIMBA DAY: HALI ILIVYO UWANJANI TAIFA MUDA HUU

Image
NancyTheDreamtz

LIVE SIMBA DAY: HALI ILIVYO UWANJANI TAIFA MUDA HUU

Image
NancyTheDreamtz

Mwanamke Kaamua Kufunga Ndoa na Mbwa Baada ya Kutembea na Wanaume 221

Image
NancyTheDreamtz Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Elizabeth Hoad raia wa Uingereza,  amefunga ndoa na Mbwa wake aitwaye Logan katika kipindi cha Television Nchini humo. Baada ya kufunga ndoa, Mwanamke huyo ameeleza aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Wanaume 221, kati ya hao Wanne ndio walimvalisha pete ya uchumba lakini imeshindikana kuolewa. Pia mwanamke huyo amesema ameamua kufunga ndoa na Mbwa wake "Logan", kwa sababu ya kuchoshwa na Tabia za Wanaume wazee kupenda Wanawake wadogo na Wanawake wadogo kupenda Wanaume wazee. Aidha Elizabeth ameendelea kusema Mbwa huyo ana maana kubwa sana kwake kwa sababu wameshasaidiana kwa vitu vingi hasa wakati alipoumizwa na Wanaume ambao aliwahi kuwa nao, pia ana marafiki zake 10 ambao wameamua kufunga ndoa na Mbwa wao. Akiweka kiapo katika sherehe ya kufunga ndoa hiyo Elizabeth aliahidi kuwa, "kwa mwili wake wote atatembea na Mbwa Logan, atamjali na kumpenda siku zote za maisha yake na kulala nae kitanda kimoja" amese...

Wakazi wa Mtwara Watakiwa Kuongeza Kasi ya Uzalishaji wa Mazao

Image
NancyTheDreamtz Wakazi wa mkoa wa Mtwara wametakiwa kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ili waweze kutumia vizuri fursa za ujenzi wa miundombinu ya barabara, anga na bandari kujiimarisha kiuchumi. Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi),Elius John Kwandikwa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha ukanda wa kusini mwa Tanzania unafunguka kimiundombinu katika nyanja za barabara za lami, bandari na usafiri wa anga hivyo kazi inayowakabili wananchi ni kuongeza uzalishaji. Akizungumza na wanakijiji wa Nanguruwe mkoani humo, Kwandikwa amesisitiza kuwa nia ya Serikali ni kuweka fursa ya miundombinu bora katika kila kanda ili wananchi waitumie kukuza uchumi binafsi na hivyo kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo 2025. “Tumejipanga kuhakikisha nyanja zote za usafiri zinaimarika katika ukanda huu wa kusini hivyo nawaomba zalisheni kwa wingi mazao ya chakula na biashara ili kufikia soko kwa haraka popote lilipo,” amesema Kwan...

Simba Yatangaza Usajili wa Mchezaji Mwingine

Image
NancyTheDreamtz Klabu ya soka ya Simba kupitia kwa msemaji wake Haji Manara ameweka wazi kuwa, leo watamtangaza mchezaji mmoja ambaye mpaka sasa alikuwa hajaungana na kikosi kwenye maandalizi ya msimu ujao. Akiongea kwenye 5SPORTS ya East Africa Television, Manara ameeleza kuwa kuna 'suprise' watu wajiandae kumjua kesho wakati akimtambulisha. ''Kuna mchezaji mpya kabisa na anacheza nafasi zote uwanjani, nitamtambulisha wa mwisho'', alisema Manara. Manara pia ameongeza kuwa, tayari kocha Patrick Aussems ameshapewa malengo ya msimu ujao wa 2019/20, ambapo anatakiwa kuhakikisha timu inatetea ubingwa wa ligi kuu kisha kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba leo wanaadhimisha tamasha lao la 'Simba Day' ambapo linafanyika kwa mara ya 10 mfululizo ikiwa ni maalum kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kutambulisha wachezaji watakaowatumia msimu mzima.

Makombora mapya ya 9M729 ya Urusi yanayoitia tumbo joto Marekani na washirika wake

Image
NancyTheDreamtz Marekani inatarajiwa kujitoa rasmi katika mkataba wa nyuklia na Urusi, hatua inayozusha hofu kuhusu ushindani wa silaha mpya. Mkataba huo unaohusu zana za nyuklia za masafa ya katikati (INF) ulisainiwa na rais wa Marekani Ronald Reagan na kiongozi wa iliyokuwa Sovieti Mikhail Gorbachev mnamo 1987. Ulipiga marufuku makombora ya masafa ya kati ya kilomita 500-5,500. Lakini awali mwaka huu Marekani na Nato ziliishutumu Urusi kwa kukiuka makubaliano hayo kwa kufyetua aina mpya ya kombora, jambo ambalo Moscow inalikana. Marekani imesema ina ushahidi kuwa Urusi imetuma kombora aina ya 9M729 linalofahamika kwa Nato kama SSC-8. Tuhuma hizi ziliwasilishwa kwa washirika wa Nato wa Marekani ambao wote waliunga mkono madai ya Marekani Rais Donald Trump mnamo Februari alitangaza kuwa Marekani itajitoa kutoka mkataba huo iwapo Urusi haitotii, na kuweka tarehe ya mwisho kuwa Agosti 2. Rais wa Urusi Vladimir Putin na yeye  amesitisha majukumu ya taifa lake katika mkataba huo mu...

Serikali Yapongezwa Mfumo Wa GePG

Image
NancyTheDreamtz Na. Peter Haule na Farida Ramadhani, WFM, Simiyu Mwandishi Mashughuli wa Vitabu nchini kikiwemo cha “Mabala The Farm”, Bw. Richard Mabala, ameipongeza Serikali kwa kubuni mfumo wa kielektroniki wa makusanyo ya maduhuli ya Serikali- GePG kwa kuwa unasaidia kudhibiti ubadhilifu wa fedha za umma na kuweka uwazi wa mapato na matumizi. Alibainisha hayo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. Alisema kuwa Mfumo wa GePG unamanufaa kwa Serikali na wananchi, kutokana na uwazi uliopo lakini pia makusanyo kufika kwa wakati katika maeneo husika kwa ajili ya matumizi ya maendeleo na mengine. “Mfumo huo utanisaidia malipo ya kodi ya majengo na kodi nyingine kwa kuwa unaondoa urasimu wa kwenda katika ofisi mbalimbali kwa ajili ya malipo na pia unaokoa muda kwa kuwa ni rahisi kuutumia kwa njia ya simu ya mkononi”, alisema Bw. Mabala. Mwandishi huyo wa Vitabu a...

Rais Magufuli: Tanzania Tunao Uwezo Wa Kutekeleza Miradi Mikubwa Ya Maendeleo

Image
NancyTheDreamtz RAIS Dkt. John Magufuli amesema Tanzania ina uwezo mkubwa wa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo nchini pasipo na kutegemea fedha zenye masharti zinazotolewa kutoka kwa wafadhili na wadau wa kimataifa wa maendeleo. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la 3 la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi (Agosti 1, 2019), Rais Magufuli alisema uzinduzi wa Jengo la Uwanja huo ni ushahidi wa wazi wa usimamizi na nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali zinazotokana na kodi ya wananchi. Aliongeza Jengo la Uwanja huo limejengwa kwa asilimia 100 kutokana na kodi za Watanzania, na hivyo kuiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD) kusimamia vyema miundombinu ya Uwanja huo kwa kuhakikisha kuwa inatunzwa ili kuakisi vyema taswira ya Jiji la Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla. Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema jengo hilo litakalokuwa na uwezo wa kuhudumia jumla ya abiri...

Tanzania Yajiandaa Kupokea Ugeni Wa Kutoka Jumuiya Ya Nchi Wanachama Kusini Mwa Afrika (SADC).

Image
NancyTheDreamtz Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara  Profesa Joseph Buchweishaija amewataka watanzania wote kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maadhimisho na maonyesho ya nne ya wiki ya Viwanda ya Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Africa (SADC) .  Maadhimisho na Maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 8 Agosti 2019 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC); Viwanja vya Karimjee na Gymkhana jijini Dar es Salaam. Profesa Bucheishaija amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara inawaalika wananchi kufika kwa wingi kwani tunatarajia jumla ya nchi  15 wanachama wa SADC zitashiriki, Aidha, ameongeza kuwa wiki hii ya SADC itawawezesha wananchi kuona fursa mbalimbali ikiwemo kuweza kupata malighafi za kilimo ambazo viwanda utumia kuzalisha bidhaa za viwandani. Miongoni mwa faida watakazozipata watanzania kupitia maonesho ya Viwanda kwa nchi za Kusini mwa Afrika  ni pamoja na kujifunza au kubadilishana uzoefu n...

Rais Magufuli apiga ‘push-up’ Tena Dar

Image
NancyTheDreamtz Rais  wa Tanzania, John Magufuli leo Alhamisi Agosti Mosi, 2019 amepiga ‘push-up’ tisa kabla ya kuzindua jengo jipya la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). Katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015, ilikuwa ni kawaida kumshuhudia Rais Magufuli akipiga ‘push-up’ katika mikutano yake mbalimbali hali iliyotafsiriwa kuwa yuko imara kuwatumikia Watanzania. Leo amerudia tena wakati akiongoza viongozi walioketi meza kuu kwenda kuwatunza waimbaji wa bendi ya Tanzania One Theatre (TOT). Alipofika mbele ya wanenguaji wa bendi hiyo alisimama mbele yao kupiga  ‘push-up’ tisa na kunyanyuka hali iliyoibua shangwe kwa waliohudhuria uzinduzi huo.