Simba Yatangaza Usajili wa Mchezaji Mwingine

NancyTheDreamtz
Simba Yatangaza Usajili wa Mchezaji Mwingine
Klabu ya soka ya Simba kupitia kwa msemaji wake Haji Manara ameweka wazi kuwa, leo watamtangaza mchezaji mmoja ambaye mpaka sasa alikuwa hajaungana na kikosi kwenye maandalizi ya msimu ujao.

Akiongea kwenye 5SPORTS ya East Africa Television, Manara ameeleza kuwa kuna 'suprise' watu wajiandae kumjua kesho wakati akimtambulisha.

''Kuna mchezaji mpya kabisa na anacheza nafasi zote uwanjani, nitamtambulisha wa mwisho'', alisema Manara.

Manara pia ameongeza kuwa, tayari kocha Patrick Aussems ameshapewa malengo ya msimu ujao wa 2019/20, ambapo anatakiwa kuhakikisha timu inatetea ubingwa wa ligi kuu kisha kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba leo wanaadhimisha tamasha lao la 'Simba Day' ambapo linafanyika kwa mara ya 10 mfululizo ikiwa ni maalum kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kutambulisha wachezaji watakaowatumia msimu mzima.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele