Skip to main content

Harmonize akutana na Meneja wa TI & Travis Scott, uongozi wake waahidi mambo makubwa (+Audio)

NancyTheDreamtz
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize amekutana na meneja wa wasanii maarufu nchini Marekani, Jason Geter na uongozi wake umezungumzia tukio hilo.
Harmonize na Jason Geter
Akiongea na Bongo5, Meneja wa Harmonize, Mr Puaz amesema kuwa wapo Marekani kupiga show kwenye baadhi ya miji mbalimbali, lakini pia kupanua wigo wa Bongo Fleva nchini Marekani.
Mr Puaz na Jason Geter
Mr Puaz amesema kuwa leo amekutana na meneja Jason Geter na wamefanya mazungumzo ya kikazi huku akiwaahidi mashabiki wa Harmonize kukaa mkao wa kula.
Jason Geter  kwa sasa anawameneji wasanii wakubwa wawili nchini Marekani ambao ni TI na Travis Scott.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele