Irene Uwoya Adai Kuwa Hataki Kuolewa Tena

NancyTheDreamtz
Msanii wa Bongo movie na mjasiriamali Irene Uwoya ameibuka na kuweka wazi kuwa hakuna kitu hataki kusikia maishani Mwaka kwa Hivi sasa Kama kuolewa tena au ndoa.
Uwoya amefunguka na kusema kuwa amefikia kwenye uamuzi huo kwani aliyokutana nayo ndani ya ndoa yameshatosheleza moyo wake hivyo kwa sasa yupo kwa ajili ya kuangalia maisha yake na si vinginevyo.

Katika mahojiano yake aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Uwoya alisema kuna vitu vingi anavyo moyoni, lakini pia anaona siyo vyema kuwapa watu faida na ndiyo maana alikuwa anakaa kimya kwa muda mrefu tangu kusambaa kwa habari zake za kuachana na Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’.

Kiukweli kabisa nimeapa moyoni mwangu sitaki kabisa kusikia kama kuna kitu kinaitwa ndoa kwa sababu nahisi hivyo vitu kwenye maisha yangu vimeshapita, sihitaji kuvirudia, naangalia maisha mengine ya kujiendeleza mwenyewe.

Kama sasa hivi nina kazi kubwa ya kumalizia pub (baa) yangu ya Last Minute (ipo Sinza-Mori, Dar). Kwa hiyo akili yote imeahamia huko”.



Irene Uwoya ameshaolewa ndoa mbili ambapo ndoa ya kwanza ilikuwa na Marehemu Ndikumana ambaye alizaa naye Mtoto mmoja na ndoa ya pili ilikuwa na Staa wa Bongo fleva Dogo Janja ambaye wameachana mapema mwaka huu Baada ya tetesi za kutokuwa na uaminifu.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele