Nilitamani kuwa mwanajeshi – Mbwana Samatta

NancyTheDreamtz
Mshambuliaji hatari ndani ya klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji raia wa Tanzania, Mbwana Samatta amesema kuwa kabla ya maisha yake ya soka alitamani kuwa mwanajeshi.
Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram huku akiwaacha washabiki wake na swali.
Muda mwingine mungu akupi unaloliomba ila anakupa linalo kustahili…
Kabla ya soka,nilikuwa natamani kuwa mwanajeshi,je kwa sura hii unadhan ningependeza kuwa soja?
Kwa sasa nyota huyo yupo njiani akielekea nchini Uganda akiwa na wachezaji wenzake wa Taifa Stars kwaajili ya kuikabili timu ya Uganda ‘The Cranes’ ikiwa ni mchezo wa kuwania kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon utakao pigwa siku ya Jumamosi ya Septemba 8 mwaka huu 2018.


Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele