Alikiba kuchafua hali ya hewa? mashabiki watabiri neema

NancyTheDreamtz
Msanii wa muziki Alikiba baada ya ukimya wa muda mrefu ame-teaser picha inayodaiwa kuwa ni screenshot ya video yake mpya.
Muimbaji huyo toka aachie ‘Mvumo Wa Radi’ mwezi May mwaka huu alikuwa kimya lakini baadaye alikuja na project ya Mofaya.
Ali ambaye aliingia kwenye maisha ya ndoa miezi miwili iliyopita, alijitupa tena kwenye maisha ya soka baada ya kuwa mdhamini mkuu wa timu ya ligi kuu ya Coastal Union ya Tanga kupitia kinywaji chake cha Mofaya.
Alhamisi hii amepost screenshot ya picha mtandaoni ambayo mashabiki wengi wa muimbaji huyo wanadai kuwa huwenda ikawa ni project mpya.
Mapema mwezi uliopita Bongo5 ilipiga stori na mdogo wa muimbaji huyo, Abdul Kiba na kudai project ambayo inakuja atashirikiana na kaka yake wakiiwakilisha label ya King Music.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele