Emmanuel Mbasha Amcharua Shilole, Amtaka Afanye Kazi Asitie Huruma kwa Rais Magufuli

NancyTheDreamtz
Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Emmanuel Mbasha ameamua kuwatolea uvivu watu wote maarufu wanaomuandama Rais Magufuli kwa kutaka msaada wa mali ile hali wana uwezo kifedha, akiwemo msanii wa muziki nchini Tanzania, Shilole.

Mbasaha amesema kuwa Slogan ya Rais Magufuli ni ‘Hapa Kazi Tu’ huku akimshangaa msanii mkubwa kama Shilole kubitaji msaada wa ada ya kumsomesha mtoto wake ile hali anafanya kazi na ni mjasiriamali.

 “Habari za mda huu . Naandika kwa masikitiko makubwa sana juu ya watu wanaopenda kutumia vibaya huruma ya raisi wetu, haswa wasanii wa bongo movie. Jamani sera ya raisi wetu ni kila mtu afanye kazi na ndiyo maana slogan yake inasema “HAPA KAZI TU” Ukifanya kazi na kujituma kama sisi mbona maisha ni mazuri tu hapa Tanzania jamani, ila ukipenda mteremko ndiyo inaweza kuku cost 😁😁😁😁. Dada yangu Shilole, yaani juzi tu umepost bonge la jumba hapa kila mtu akafurahia na kukupongeza hadi mie nilikupongeza, japokuwa wiki moja kabla ya hapo kuna kijana alikuwa anadai pesa zake za pili pili😭.😭😭😭. Leo nileshangaa kuona clip inasambaa ukilia na kuomba raisi akusaidie kukusomeshea mtoto, sitaki kukupinga ila nakuuliza na kukushauri. Jambo ambalo nakuuliza ni kwamba, Je ! Umesahau kuwa elimu ni bure kuanzia chekechea hadi form four ? Je ! Huyo unaetaka asomeshwe yuko darasa la ngapi dada yangu? Mimi nadhani vitu vingine tungevipima kabla ya kuamua kuchukua hatua. Hebu jiulize, leo raisi akikulipia ada ya mwanao unadhania hawa watoto wa maskini kabisa ambao hawana hata makazi watajisikiaje kama sio kutaka kubebeshana lawama ??,“ameandika Emmanuel Mbasha kwenye ukurasa wa Instagram na kutoa ushauri kwa wasanii.

 “Mimi nadhani wasanii tutumie majina yetu kusaidia jamii isiyojiweza na sio kutafuta mteremko. Kweli marafiki zako wote umeshindwa hata kuwakopa kimya kimya hiyo pesa ya ada kisha uwarejeshee kidogo kidogo pale biashara inapokwenda sawa ? Mimi nadhani hichi ulichokifanya ulistahili kukifanya kwa niaba ya mtu ambaye hana jina wala connection kama zako ili utumie jina lako kumuombea msaada kwa raisi, na siyo mwanamke mpambanaji kama wewe.mie nadhani ungeandika andiko ambalo ungempelekea raisi na ukaomba akudhamini ili upate pesa Bank 400 Ml au Zaidi ukakopeshwa na ukafungua hotel kubwa na pia utakua umetengeneza ajira kwa vijana wenzetu kuliko hilo wazo,Pia kumbuka juzi tu tulikuwa na msiba kule Chato nadhani badala ya kuibuka leo na kutaka msaada angarau ungejitokeza na rambirambi kidogo ili ikuwekee mazingira mazuri ya kuja kukiwakilisha hichi kilio chako hapo baadaye. Haya ni maoni yangu kama Mtanzania huru, sitaki povu hapa jamani. Kamati yangu ya kublock kaeni mkao wa kura.kama unaweza kuzunguka na Ttcl nchi nzima.kajifunze kwa @munalove100 basi,“ameeleza Mbasha.

Kwa upande mwingine Shilole amemjibu kwa kusema
 “Nakuheshimu sana kaka yangu please tulinde heshima yetu”.

Wiki mbili zilizopita Shilole alikaririwa kwenye vyombo vya habari akiomba msaada kwa Rais Magufuli wa kumsomesha mtoto wake mmoja wa kike ambae amedai kuwa baba yake mzazi amefariki dunia.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele