Harmonize achafua hali ya hewa mtandaoni, Barnaba na Eugy kutoka Ghana watoa baraka zao (+video)

NancyTheDreamtz
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize amekuwa gumzo mitandaoni kwa siku ya leo Tanzania baada ya kutangaza kuwa anaachia ngoma mpya.
Harmonize
Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram amewaahidi kuwa ataachia video ya wimbo wake mpya endapo atatapata maoni (Comments) zaidi ya 2000.

Posti hiyo mpaka sasa imeshangaa masaa manne na tayari imefikisha comments 3000+ na views 102,000+ na kinachofuatia sasa ni mashabiki wake kumuandama mitandaoni mkali huyo wa Kwangwaru kuachia kichupa hicho.
Wengine waliotoa neno juu ya ujio wa ngoma hiyo ni mwanamuziki Barnaba na Eugy kutoka nchini Ghana ambao nao wamedai kuwa wimbo huo utakuwa ni moto wa kuotea mbali.
Aiseee hili chuma, chuma naikumbuka mzee balaa sana ni chuma na nusuu,“ameandika Barnaba huku msanii wa muziki kutoka Ghana, Eugy akiandika “Let’s goooo!!“.
Ngoma hiyo mpya ya Atarudi ni ngoma ya tatu ya Harmonize kufanya kwa mwaka huu baada ya ngoma yake ya DM Chick na Kwangaru aliyomshirikisha Diamond Platnumz kufanya vizuri.
Je, Atarudi huenda ukawa wimbo mkubwa na mkali zaidi ya Kwangwaru na DM Chick?

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele