Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele
Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele YANGA wanahitaji sana duma ya mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube. Wanaamini Dube anaweza kuwa mtu sahihi wa kuziba nafasi ya Fiston Mayele. Inaaminika kwamba Yanga wamekuwa wakihangaika kumshawishi mchezaji huyo kwa muda mrefu kutua katika kikosi hicho kutokana na uwezo wake. . Hivi karibuni wakati Azam FC ikiwa mikoani kwa mechi za Ligi Kuu, Dube alionekana kwenye Uwanja wa Mkapa akishuhudia mechi ya Yanga ambapo ilishinda mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad. Dube hakusafiri na Azam kwa sababu ni majeruhi ambapo amekosa michezo kadhaa hadi sasa. . Nyota huyo hajacheza mechi ya Azam FC tangu Februari 19 alipoingia kipindi cha pili dhidi ya Tabora United. Hakusafiri na timu katika mechi mbili za mikoani Mbeya dhidi ya Prisons na Mwanza dhidi ya Singida. Lakini ARENA ltuajua kwa kawaida Azam FC husafiri na wachezaji wake hata kama ni majeruhi kama sehemu ya kujenga umoja. Hata hivyo Dube hakusafiri ikisemekana ali...