Posts

Simba yaanza mipango, kuimaliza Kaizer Chiefs

Image
Kikosi cha Simba SC kitaingia kambini kesho tayari kwa maandalizi kuelekea mchezo wa mkondo wa pili war obo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs mchezo utakao chezwa siku ya Jumamosi Mei 22, 2021 katika dimba la Mkapa Dar es salaam. Kikosi hicho cha mabingwa wa Tanzania bara kimerejea nchini leo kikitokea Afrika Kusini ambako kilicheza mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika, mchezo ambao wekundu hao wa msimbazi walipoteza kwa kufungwa mabao 4-0, mchezo ambao ulichezwa katika dimba la FNB. Baada ya kikosi hicho kurejea mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo Haji Sunday Manara alieleza juu ya mipango ya kikosi hicho kuelekea mchezo huo wa Jumamosi, “Kesho asubuhi ndo tunaanza mazoezi na Camp moja kwa moja, tunamshukuru mwenyezi Mungu mpaka sasa hivi hatuna majeruhi mpya na baada ya leo kupumzika tutazungumza na waandishi kuelezea mikakati kinachoendelea kama klabu lakini kwa hivi sasa wache...

Gomes: Tutawashangaza Kaizer Kwa Mkapa

Image
WAKATI wadau wengi wa soka wakiamini kuwa ndoto za Simba kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika zimeyayuka kufuatia kichapo cha mabao 4-0, lakini hali hiyo ni tofauti kwa Kocha Didier Gomes ambaye anaamini kuna maajabu yatatokea kwa Mkapa. Gomes alisema raha ya mpira ni sayansi iliyopo wazi, kwani kama kuna watu waliamini watashinda ugenini au kutoka sare na mwishowe wakafungwa, basi hata kwa Mkapa kuna matokeo yasitarajiwa na wengi yanaweza kutokea. Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa wa Afrika Kusini, Soccer City Gomes alisema licha ya kupoteza kwa mabao mengi haina maana kuwa walicheza vibaya. “Tulifungwa siyo kwa sababu hatukucheza vizuri, tulikuwa bora uwanjani na tulifanya kila kitu tulichopanga ila bahati haikuwa kwetu na ile ndiyo tafsiri ya soka, hakuna ambaye anaweza kulitabiri.“ Hatujatolewa kwenye mashindano kwa sababu bado tuna dakika 90 zingine tukiwa Dar es Salaam, naamini kuna jambo...

Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? Jibu Lake Hili Hapa Hakika Litakushangaza

Image
NancyTheDreamtz Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani. Kwa mujibu wa Einstein kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa vyao vinabaki vitupu. Kitu pekee walichojaza kichwani ni yale waliyofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu. SHINDA ZAWADI YA SIMU KWA KUDOWNLOAD APPP YA UDAKU SPECIAL  HAPA Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili. Icons wa Sayansi kama Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia. Akili siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Y...

Waliosambaza Video Chafu, za Denti Chuo Kikuu, Jela Miaka 3…

Image
‘CONNECTION’ ndiyo msemo unaotrend (sambaa) kila kona ya jiji la Dar, baada ya video chafu ya mwanadada mmoja anayedaiwa kuwa ni denti wa Chuo Kikuu (jina linafi chwa) jijini Dar es Salaam, kuvujishwa na marafi ki zake.   Kufuatia kuvuja kwa video hiyo chafu, kila mtu anaomba kutumiwa video hiyo na kisha naye kuisambaza, jambo ambalo Jeshi la Polisi nchini, limeonya kuwa mkono wa sheria utafuata dhidi yao. Tukio hilo limesababisha kuibuka kwa taarifa mbalimbali huku mhanga wa video hiyo akidaiwa kunywa sumu na kufariki dunia.   TUKIO LILIVYOANZA Tukio hilo lilianza kusambaa kama moto wa kifuu juzi jioni, huku kila mmoja akieleza chanzo chake, lakini kwa mujibu wa rafi ki wa karibu (shogaye) wa mlimbwende huyo ambaye alijitambulisha kuwa wanasoma wote katika chuo hicho, alimwaga mkanda mzima na kudai kuwa, shoga yake huyo hajafariki.   “Huyu dada anasoma chuo kikuu cha (anakitaja), alikuwa na mpenzi wake ambaye kwa sasa wameshaachana. Kipindi wapo kwenye uhusiano wa kimape...

Msanii Mario Ataka Kujinyonga KISA Mimi Mars Kuchukuliwa na Diamond Platnum

Image
Msanii Mariko amechukua jukumu la kutaka kujinyonga baada ya kupata tetesi ya aliekuwa mpenzi wake mimi Mars kutoka na msanii diamond platnum Kimapenzi   NancyTheDreamtz

Bumbuli Afunguka Sababu ya Kulipa Faini ya TFF

Image
MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Hassan Bumbuli amefunguka kuwa kuchelewa kulipwa kwa faini yake kumetokana na kusubiri kupata barua ya hukumu yake ambayo ameipata Jumatatu ya wiki hii. Bumbuli ametoa kauli hiyo baada kuchelewa kulipa faini ya Sh milioni tano iliyotokana na kutoa taarifa za uongo na upotoshaji katika suala la lililohusu shauri la aliyekuwa kiungo wa Yanga Mghana, Bernard Morrison ambapo alisema Yanga haijapewa nakala ya hukumu ya shauri la Morrison huku akifahamu kwamba nakala hiyo ilichukuliwa siku moja kabla. Bumbuli amesema kuwa, katika suala hilo hawezi kukurupuka kwenda kulipa bila ya kupata barua ya hukumu ambayo ameipokea Jumatatu ya wiki hii pamoja na kujua taratibu zengine za kufanya malipo hayo kabla ya kuomba muongozo wa kufuata kwa ajili ya kufanya malipo. “Huwezi kukurupuka kwenda kulipa, TFF wametoa hukumu na katika hukumu walisema rufaa ipo wazi lakini kuna utaratibu ndiyo unaweza kuchukua uamuzi wa kwenda kulipa au kukata rufaa, yaani hu...

Kamati ya Maadili - NEC Yasisitiza Adhabu Aliyopewa Tundu Lissu ni SAHIHI na ni Lazima Aitekeleze

Image
Kamati ya maadili ya taifa imesisitiza kuwa adhabu iliyotolewa na kamati hiyo kwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Mhe.Tundu Lissu ni sahihi na haruhusiwi kupanda kwenye jukwaa lolote la siasa hadi adhabu hiyo iishe. Hayo yamesemwa leo Jumamosi, Oktoba 3, 2020 na Katibu Kamati ya Maadili ya Kitaifa, Emmanuel Kawishe wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea sakata hilo ikiwa ni siku moja tangu Lissu asimamishwe kufanya kampeni zake kwa siku saba kwa madai ya kukiuka taratibu na kanuni za uchaguzi. “Kwa kuzingatia taratibu, Tume hupeleka taarifa kwa Katibu wa chama husika, Tume haimpelekei taarifa mgombea mmoja mmoja, Tume inawasiliana na Katibu Mkuu na si vinginevyo.  "Katibu Mkuu CHADEMA ndiye aliyemdhamini Tundu Lissu kuwa mwanachama na mgombea wa kiti cha rais kupitia chadema kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977. Hivyo, Adhabu hiyo inatakiwa kutekelezwa kwa kuwa imetolewa na chombo chenye mamlaka ya kisheria na kwa kuzingati...