Simba yaanza mipango, kuimaliza Kaizer Chiefs



Kikosi cha Simba SC kitaingia kambini kesho tayari kwa maandalizi kuelekea mchezo wa mkondo wa pili war obo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs mchezo utakao chezwa siku ya Jumamosi Mei 22, 2021 katika dimba la Mkapa Dar es salaam.

Kikosi hicho cha mabingwa wa Tanzania bara kimerejea nchini leo kikitokea Afrika Kusini ambako kilicheza mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika, mchezo ambao wekundu hao wa msimbazi walipoteza kwa kufungwa mabao 4-0, mchezo ambao ulichezwa katika dimba la FNB.


Baada ya kikosi hicho kurejea mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo Haji Sunday Manara alieleza juu ya mipango ya kikosi hicho kuelekea mchezo huo wa Jumamosi,


“Kesho asubuhi ndo tunaanza mazoezi na Camp moja kwa moja, tunamshukuru mwenyezi Mungu mpaka sasa hivi hatuna majeruhi mpya na baada ya leo kupumzika tutazungumza na waandishi kuelezea mikakati kinachoendelea kama klabu lakini kwa hivi sasa wachezaji wapate mapumziko ya siku moja.”


Katika mchezo wa marejeano Simba inahitaji ushindo wa kuanzia mabao matano(5) kwa sifuri ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hii au ushindi wowote ule unao anzia tofauti ya mabao matano.

 

NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele