Posts

Makombora mapya ya 9M729 ya Urusi yanayoitia tumbo joto Marekani na washirika wake

Image
NancyTheDreamtz Marekani inatarajiwa kujitoa rasmi katika mkataba wa nyuklia na Urusi, hatua inayozusha hofu kuhusu ushindani wa silaha mpya. Mkataba huo unaohusu zana za nyuklia za masafa ya katikati (INF) ulisainiwa na rais wa Marekani Ronald Reagan na kiongozi wa iliyokuwa Sovieti Mikhail Gorbachev mnamo 1987. Ulipiga marufuku makombora ya masafa ya kati ya kilomita 500-5,500. Lakini awali mwaka huu Marekani na Nato ziliishutumu Urusi kwa kukiuka makubaliano hayo kwa kufyetua aina mpya ya kombora, jambo ambalo Moscow inalikana. Marekani imesema ina ushahidi kuwa Urusi imetuma kombora aina ya 9M729 linalofahamika kwa Nato kama SSC-8. Tuhuma hizi ziliwasilishwa kwa washirika wa Nato wa Marekani ambao wote waliunga mkono madai ya Marekani Rais Donald Trump mnamo Februari alitangaza kuwa Marekani itajitoa kutoka mkataba huo iwapo Urusi haitotii, na kuweka tarehe ya mwisho kuwa Agosti 2. Rais wa Urusi Vladimir Putin na yeye  amesitisha majukumu ya taifa lake katika mkataba huo mu...

Serikali Yapongezwa Mfumo Wa GePG

Image
NancyTheDreamtz Na. Peter Haule na Farida Ramadhani, WFM, Simiyu Mwandishi Mashughuli wa Vitabu nchini kikiwemo cha “Mabala The Farm”, Bw. Richard Mabala, ameipongeza Serikali kwa kubuni mfumo wa kielektroniki wa makusanyo ya maduhuli ya Serikali- GePG kwa kuwa unasaidia kudhibiti ubadhilifu wa fedha za umma na kuweka uwazi wa mapato na matumizi. Alibainisha hayo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. Alisema kuwa Mfumo wa GePG unamanufaa kwa Serikali na wananchi, kutokana na uwazi uliopo lakini pia makusanyo kufika kwa wakati katika maeneo husika kwa ajili ya matumizi ya maendeleo na mengine. “Mfumo huo utanisaidia malipo ya kodi ya majengo na kodi nyingine kwa kuwa unaondoa urasimu wa kwenda katika ofisi mbalimbali kwa ajili ya malipo na pia unaokoa muda kwa kuwa ni rahisi kuutumia kwa njia ya simu ya mkononi”, alisema Bw. Mabala. Mwandishi huyo wa Vitabu a...

Rais Magufuli: Tanzania Tunao Uwezo Wa Kutekeleza Miradi Mikubwa Ya Maendeleo

Image
NancyTheDreamtz RAIS Dkt. John Magufuli amesema Tanzania ina uwezo mkubwa wa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo nchini pasipo na kutegemea fedha zenye masharti zinazotolewa kutoka kwa wafadhili na wadau wa kimataifa wa maendeleo. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la 3 la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi (Agosti 1, 2019), Rais Magufuli alisema uzinduzi wa Jengo la Uwanja huo ni ushahidi wa wazi wa usimamizi na nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali zinazotokana na kodi ya wananchi. Aliongeza Jengo la Uwanja huo limejengwa kwa asilimia 100 kutokana na kodi za Watanzania, na hivyo kuiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD) kusimamia vyema miundombinu ya Uwanja huo kwa kuhakikisha kuwa inatunzwa ili kuakisi vyema taswira ya Jiji la Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla. Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema jengo hilo litakalokuwa na uwezo wa kuhudumia jumla ya abiri...

Tanzania Yajiandaa Kupokea Ugeni Wa Kutoka Jumuiya Ya Nchi Wanachama Kusini Mwa Afrika (SADC).

Image
NancyTheDreamtz Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara  Profesa Joseph Buchweishaija amewataka watanzania wote kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maadhimisho na maonyesho ya nne ya wiki ya Viwanda ya Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Africa (SADC) .  Maadhimisho na Maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 8 Agosti 2019 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC); Viwanja vya Karimjee na Gymkhana jijini Dar es Salaam. Profesa Bucheishaija amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara inawaalika wananchi kufika kwa wingi kwani tunatarajia jumla ya nchi  15 wanachama wa SADC zitashiriki, Aidha, ameongeza kuwa wiki hii ya SADC itawawezesha wananchi kuona fursa mbalimbali ikiwemo kuweza kupata malighafi za kilimo ambazo viwanda utumia kuzalisha bidhaa za viwandani. Miongoni mwa faida watakazozipata watanzania kupitia maonesho ya Viwanda kwa nchi za Kusini mwa Afrika  ni pamoja na kujifunza au kubadilishana uzoefu n...

Rais Magufuli apiga ‘push-up’ Tena Dar

Image
NancyTheDreamtz Rais  wa Tanzania, John Magufuli leo Alhamisi Agosti Mosi, 2019 amepiga ‘push-up’ tisa kabla ya kuzindua jengo jipya la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). Katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015, ilikuwa ni kawaida kumshuhudia Rais Magufuli akipiga ‘push-up’ katika mikutano yake mbalimbali hali iliyotafsiriwa kuwa yuko imara kuwatumikia Watanzania. Leo amerudia tena wakati akiongoza viongozi walioketi meza kuu kwenda kuwatunza waimbaji wa bendi ya Tanzania One Theatre (TOT). Alipofika mbele ya wanenguaji wa bendi hiyo alisimama mbele yao kupiga  ‘push-up’ tisa na kunyanyuka hali iliyoibua shangwe kwa waliohudhuria uzinduzi huo.

Chama Aongeza Mkataba Mpya Simba SC

Image
NancyTheDreamtz MFUNGAJI wa mabao ya mwisho yaliyoipeleka hatua ya makundi na Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika timu ya Simba Mzambia, Clatous Chota Chama ‘Triple C’ ameongeza mkataba mwingine wa miaka miwili ya kuendelea kuichezea timu hiyo. Huyo, ni mchezaji wa sita kwa Simba kuongezewa mkataba wengine ni John Bocco, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Aishi Manula, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Meddie Kagere. Chama alijiunga na Simba kwenye msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara akitokea Power Dynamo inayocheza ligi ya nchini huko. Taarifa ya klabu ya Simba inaeleza kuwa kiungo huyo atakuwa sehemu ya kikosi hicho hadi 2020 baada ya kuongeza mkataba huo. Simba hivi sasa ipo kwenye mikakati ya kukiboresha kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya kimataifa Afrika na kikubwa kufika hatua ya fainali baada ya msimu uliopita kufika robo fainali. Timu hiyo hadi hivi sasa tayari imefanikiwa kuwasajili wachezaji wapya watano ambao ni Beno Kakolanya, Kennedy Juma, Gerson Fraga ...

HAMISA AAPA KUTOZAA TENA BILA NDOA!

Image
NancyTheDreamtz Mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto. BAADA ya kuzaa watoto wawili kabla ya kuolewa huku kila mtoto akiwa na baba yake, mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto amefunguka kwamba kwa sasa hafikirii tena kufanya hivyo. Akipiga stori mbili-tatu na gazeti hili, mrembo huyo alisema kuwa katika maisha yake hakuwahi kuamini katika ndoa ndiyo maana akaamua kuzaa watoto wawili bila ndoa, lakini sasa anatamani kuongeza watoto wengine watano ndani ya ndoa ili atimize ndoto yake ya kuwa na watoto saba. “Sasa hivi ninahitaji mwanaume wa kufunga naye ndoa na Mungu akitujalia nizae naye watoto watano ili nitimize ndoto yangu ya kuwa na watoto saba,” alisema Mobeto. Katika watoto wawili alionao Mobeto, mmoja amezaa na msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mwingine amezaa na Mkurugenzi wa EFM na TVE, Francis Ciza‘Majizo