Posts

Waraka wa Hamisa Mobetto wagusa Hisia za wengi

Image
NancyTheDreamtz Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameelezea kile anachokabiliana nacho kwenye maisha yake kwa sasa. Hii ni baada ya maneno kuwa mengi mtandaoni kuhusu yeye, sasa ameamua kuvunja ukimya kwa kuandika waraka mrefu kiasi.  ==>>Hapa chini tumekuwekea kile alichoandika Hamisa kupitia ukurasa wake wa Instagram; "Pengine hufahamu alipotoka Hamisa Mobetto... Wacha nikufahamishe, nilianza kutambulika rasmi kwenye tasnia ya urembo mwaka 2010 baada ya kuibuka mshindi wa Miss XXL After School Bash. Njia ya mafanikio ilifunguka hapo na hatimae nilishiriki Miss Tanzania na Also Miss New World Tanzania Na Kua first Runner Up 2012. "Lakini Pia Nilifanikiwa Kushriki Miss UniAfrica na kuingia Top Ten... Safari ikaendelea na kwa kuwa urembo ni kipande cha sanaa niliingia kwa pia kwenye Bongo Movie na kucheza filamu kadhaa na huku pia nikiwa Video Vixen kwa baadhi ya nyimbo za Bongo Fleva. "Nisieleweke vibaya kwa hili, kitanda hakizai haramu... ...

Ndalichako Ataja Sababu za Wanafunzi Kukacha Hesabu

Image
NancyTheDreamtz WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amesema kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo asilimia 80 ya wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne, wamekuwa wakifeli somo la hesabu kutokana na sababu mbalimbali. Ametaja moja ya sababu kuwa ni walimu kutokuwa na mbinu za kuwavutia wanafunzi kupenda somo hilo na kuwavunja moyo pale wanapokosea. Ndalichako aliyasema hayo juzi wakati akifungua mkutano wa walimu wa masomo ya hesabu kutoka nchi 15 za Afrika, Marekani na Uingereza, ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Aga Khan kwa lengo la kujadili mbinu za kufundisha somo hilo. Profesa Ndalichako alisema sababu za wanafunzi kufeli somo hilo ni kutokana na walimu kutokuwa wabunifu wa mbinu mbalimbali za kuwafundishia hali inayosababisha kulichukia. Alisema kutokana na wanafunzi wengi kufeli, kumekuwa na uhaba mkubwa wa walimu wa somo hilo na kusema kuwapo kwa mkutano huo kutasaidia kuongeza ari kwa walimu kuwafanya wanafunzi walipende. “Ni asilimia 20 tu ya wanafun...

Kagere Atoa Siri ya Staili yake ya Kufumba Jicho

Image
NancyTheDreamtz STRAIKA mkali kwa mabao ya vichwa, Meddie Kagere ambaye mtindo wa kushangilia kwa kufunika jicho moja umewafurahisha mashabiki amesisitiza kuwa yajayo yanafurahisha.  Kagere ambaye amecheza mechi mbili za ligi kuu ametupia mabao 3 huku bao 1 akifunga dhidi ya Prisons kwa guu lake la kulia na mabao 2 akifunga kwa bichwa dhidi ya timu ya Mbeya City ambao walilala na viatu.  Akizungumza na Spoti Xtra Kagere alisema kuwa kwake mtindo wa kufumba jicho ni mtindo wa kushangilia tu na kitu kikubwa ambacho kinafanya aweze kung’ara ni ushirikiano ndani ya timu.  “Tunacheza tukiwa ni timu na kwa kufuata maelekezo ya mwalimu tunafanikiwa kupata matokeo hivyo hicho ndicho kilicho nyuma ya mafanikio yangu ambayo ni ya timu kiujumla,” anasema mchezaji huyo mzaliwa wa Uganda aliyewaacha Gor Mahia kwenye mataa.  “Kuhusu mtindo wangu wa kuziba jicho ni aina tu ya ushangiliaji haina maana yoyote na ninaipenda kwa sababu tayari mashabiki wangu wameipokea vizuri, baada ...

Cristiano Ronaldo Anasikitisha Sana, Anakwama Wapi?

Image
NancyTheDreamtz Parma 1 Juventus 2, unawaza nini unaposoma ubao wa matokeo unasoma namna hiyo? Moja kwa moja utakimbilia kuuliza Ronaldo amefunga, na jibu la hajafunga linakujia. Ni kweli bwana Mario Madzukic kama kawaida amesimamia show hii leo pamoja na Blaise Matuidi wamefunga mabao ya Juventus vs Parma na Gervinho akafunga la Parma na kumfanya Cr7 kutofunga katika mechi 3 za mwanzo Serie A. Suala la kuhuzinisha kuhusu Ronaldo ni hizi timu tatu walizokwishacheza nazo, hizi ni timu ambazo kweye makaratasi zonaonekana ni nyepesi sana. Hivi kwa mfano Chievo, msimu uliopita walimaliza nafasi saba kutoka mwisho tena walimaliza msimu wakiwa na goal difference ya mabao 23, Ronaldo hakuwafunga. Lazio, kama hujui tu nikuambie Lazio msimu uliopita katikaashindano yote walifungwa mabao 70, ni timu ambayo ina ulinzi dhaifu lakink Ronaldo hakufunga. Parma hawa hadi mwaka 2016 walikuwa Serie D huko, 2015 walikumbwa na tatizo kubwa la kipesa wakafilisika, na mwaka huu ndio wamepanda Serie A, ...

MASKINI..Gari ya Watalii yapata Ajali Mbaya Arusha

Image
NancyTheDreamtz Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (SACP) Ramadhani Ng’anzi, amethibitisha kutokea kwa ajali ya gari  iliyohusisha Lori na gari ya kubeba watalii. Ajali hiyo imetokea eneo la Mti mmoja Wilayani Monduli. Kamanda Ng’anzi amesema gari aina ya Land Cruiser iliyokuwa imebeba watalii imegongana uso kwa uso na Lori la mizigo takribani Kilometa 10 kutoka njia panda ya Monduli. ”Nipo eneo la ajali hapa muda huu, tunaendelea na vipimo hapa, nitawajulisha kwa undani lakini vifo vipo ila bado hatujajua ni idadi gani”, amesema. Taarifa za awali zinaeleza takribani watu watano wamefariki katika ajali hiyo. Endelea kufuatilia Udaku Special tutakujuza zaidi juu ya ajali hiyo.

Madiwani wengine wa Chadema Arusha watimkia CCM usiku

Image
NancyTheDreamtz Kimbunga cha madiwani na wabunge kuhama hasa vyama vya upinzani na kuhamia CCM kimeendelea kutimka, ambapo jana usiku madiwani wengine wawili wa jiji la Arusha walifuata mkondo. Madiwani hao walioshinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chadema, jana usiku walitangaza kujiuzulu nafasi zao na kujiunga na CCM hivyo kufanya idadi ya madiwani wa Arusha waliochukua hatua hiyo kufikia wanane. Wakizungumzia sababu za kujiuzulu, Alex Marti wa kata ya Olasitin na Amani Liwadi wa kata ya Engutoto, wamesea lengo ni kumuunga mkono Rais John Magufuli. “Nimeamua kwa ridhaa yangu mwenyewe kujiuzulu udiwani. Nimeandika barua kwa viongozi wa Chadema kueleza uamuzi wangu, kikubwa kilichofanya niamue hivi ni kazi nzuri inayofanywa na Rais John Magufuli,” alisema Marti. Liwadi pia alitoa sababu sawa na za Marti na kwamba tayari ameandika barua kwenda Chadema. Uamuzi huo wa madiwani hao unaifanya Chadema kubaki na madiwani 25, huku madiwani wa CCM wakiwa saba kutoka idadi ya madiwani...

Kutoonekana’ Makontena 10 ya Makonda Mnadani Kwazua Jambo

Image
NancyTheDreamtz Kwa mara nyingine jana makontena 20 ya Paul Makonda yalikosa mnunuzi bandarini, licha ya matumaini ya awali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa kulikuwa na dalili nzuri zaidi kuliko wiki iliyopita, huku idadi ikizua jambo. Baadhi ya watu waliokuwa wanashiriki katika mnada huo walieleza kuwa kuonekana kwa makontena 10 pekee katika siku ya mnada badala ya makontena yote 20 ni moja kati ya vitu vilivyozua wasiwasi. Akijibu kuhusu kutoonekana kwa makontena mengine 10 kwenye mnada huo ulioanza majira ya saa tatu asubuhi, afisa mwandamizi wa TRA ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema hilo pamoja na mambo mengine lilitokana na ufinyu wa nafasi ya eneo la mnada. “Tulifikiria pia ukweli kuwa washiriki wote wa mnada walipewa siku tatu kuyaangalia makontena yote 20 na bidhaa zilizomo, hivyo hatukuona haja ya kuyabeba tena yote 20,” The Citizen inamkariri. Aidha, suala la bei lililalamikiwa pia na baadhi ya washiriki wa mnada huo uliokuwa ukifanywa na kampuni ya Yono Auc...