Posts

Showing posts from October, 2021

Inachekesha..Wamarekani Hawamfahamu Diamond, Wazani ni Mchezaji Mpya wa Timu yao

Baada ya Timu ya @washingtonnfl kumzawadia Jezi na kumpost @diamondplatnumz kwenye page yao ya Instagram, mashabiki wa timu hiyo wameonekana kushangazwa na mtu huyu, huku wengi wakijua ni mchezaji mpya wa timu yao. Maswali mengi yameibuka kutoka kwa mashabiki hao mfano "Who?", "Who is that?" "Can he play" "Can he Help our Team", "Serious Question who is this" Baadhi ya wabongo na waafrika wameonekana kujibu baadhi ya comments za wamarekani kwa kusema kwamba huyu ni msanii kutoka Afrika, East Africa na Wengine wakaitaja Tanzania. Kumbe wasanii wetu Usikute Show zao za marekani huwa wanahudhuria wabongo tu labda na wakenya wa huko, maana hili jambo limeonesha wazi kuwa wasanii kutoka Tanzania hawafahamiki, yani wanajua mchezaji mpya kasajiliwa nyandichethedreamtz

Miquissone “Simba ilinipa jina kubwa katika soka Afrika"

“Simba ilinipa jina kubwa katika soka Afrika, hapo kabla sikucheza hatua ya robo fainali klabu bingwa Afrika nimefanya hivyo nikiwa na Simba, ni heshima kubwa kwa mchezaji yeyote mwenye kiu ya mafanikio” 🗣“Simba Sc ilinilea vyema na ninaamini ipo siku nitarejea kama itakuwa sehemu ya mipango ya Mungu” nyandichethedreamtz

Kilichomuondoa Antonio Nugaz Yanga Huenda ni Hichi

"Wakati naingia Young Africans niliwaambia viongozi msije mkamfukuza mtu yeyote, Mkifanya hivyo itaonekana Mimi ndio nimehusika katika hilo. "Kile alichokifanya Nugaz kunitusi bila sababu inawezekana kabisa kuwa ndicho kilichomuondoa Nugaz." "Mimi sijakukosea kitu unanitusi vipi! Nimeingia Young Africans Siku ya pili tu unanitusi bila sababu, sijawahi kukuosea!" - Haji Manara, Msemaji wa Young Africans nyandichethedreamtz

Mo Dewji "Napata Hasara Simba Napoteza Hela Nyingi Sana"

MFANYABIASHARA maarufu Tanzania na Afrika kwa ujumla ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo Dewji’ akihojiwa na Shirika la Utangazaji la CCN nchini Marekani amesema amewekeza kwenye klabu ya (10) kwa ubora Barani Afrika na ina mashabiki Tsh milioni 40. Amesema pesa zake zinapotea kwani hapati faida, mpaka sasa ametumia zaidi ya dola za Kimarekani milioni 20 bila kupata faida, lakini amewekeza kutokana na mapenzi tu, lakini klabu hiyo haimuingizii faida yeyote. “Simba SC ina miaka 85, ina mashabiki 40m, ndani ya miaka 4 nimewekeza dola milioni 20 ili iwe miongoni mwa klabu 10 bora Afrika. Tuna malengo makubwa. Hakuna biashara ila napoteza hela nyingi. Nafanya haya kwa mapenzi yangu sababu naipenda sana Simba,” amesema Mo Dewji. nyandichethedreamtz