Ifahamu Siku ya Ijumaa Kuu Kiundani...

NancyTheDreamtz


Siku kama ya leo saa tisa alasiri, ni maarufu kama Ijumaa Kuu, katika nyumba za ibada za Kikristo, kimya hutanda, mishumaa huzimwa na kuashiria kuwa ni siku ya majonzi. Ijumaa Kuu ni siku ambayo Wakristo duniani kote hukumbuka mateso aliyoyapata Yesu


Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimeipa thamani siku hii kwa kuitangaza kuwa ya mapunziko. Siku hii huadhimishwa kwa ibada inayoambatana na kusoma mistari ya Biblia inayoelezea undani wa matukio yaliyosababisha kusulubiwa kwa Yesu Kristo miaka zaidi ya 2000 iliyopita.

Hii ni siku ambayo inatajwa kuwa na maana kubwa katika imani ya Kikristo. Waumini wanaamini kwamba, kusulubiwa na kufa kwa Yesu, kumeleta ukombozi duniani kote.

Ijumaa Kuu haithibitishwi tu na vitabu vya dini, bali hata machapisho ya kihistoria, yanathibitisha juu ya kusulubiwa na kufa kwa Yesu. Huadhimishwa kwa ibada huku zikitawaliwa na mistari na nyimbo za maombolezo ya kufa kwa Yesu.

Rangi za vitambaa vipambwavyo kanisani, huwa ni zile zinazoashiria maombolezo. Hufanyika tangu asubuhi na inapofika saa tisa, muda unaosadikiwa kuwa ndipo Yesu alikata roho, makanisa hutawaliwa na kimya kiambatanacho na kuzima mishumaa ndani ya kanisa.

Katika muda huo wengi hutafakari namna walivyokombolewa kwa damu ya Yesu. Makanisa mengi, vikundi mbalimbali kama vile watoto, vijana na wanawake, hutumia siku hiyo kuonesha maigizo ya kusulubiwa na kufa kwake.

Aidha Kipindi hiki watu wengi wamejiwekea utaratibu wa kufunga kila Ijumaa wakati wengine hufunga siku 40 kabla ya Pasaka. Suala la kufunga linaloambatana na kutenda yaliyo mema, halina muda wala kikomo

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele