Posts

Showing posts from 2020

Waliosambaza Video Chafu, za Denti Chuo Kikuu, Jela Miaka 3…

Image
‘CONNECTION’ ndiyo msemo unaotrend (sambaa) kila kona ya jiji la Dar, baada ya video chafu ya mwanadada mmoja anayedaiwa kuwa ni denti wa Chuo Kikuu (jina linafi chwa) jijini Dar es Salaam, kuvujishwa na marafi ki zake.   Kufuatia kuvuja kwa video hiyo chafu, kila mtu anaomba kutumiwa video hiyo na kisha naye kuisambaza, jambo ambalo Jeshi la Polisi nchini, limeonya kuwa mkono wa sheria utafuata dhidi yao. Tukio hilo limesababisha kuibuka kwa taarifa mbalimbali huku mhanga wa video hiyo akidaiwa kunywa sumu na kufariki dunia.   TUKIO LILIVYOANZA Tukio hilo lilianza kusambaa kama moto wa kifuu juzi jioni, huku kila mmoja akieleza chanzo chake, lakini kwa mujibu wa rafi ki wa karibu (shogaye) wa mlimbwende huyo ambaye alijitambulisha kuwa wanasoma wote katika chuo hicho, alimwaga mkanda mzima na kudai kuwa, shoga yake huyo hajafariki.   “Huyu dada anasoma chuo kikuu cha (anakitaja), alikuwa na mpenzi wake ambaye kwa sasa wameshaachana. Kipindi wapo kwenye uhusiano wa kimape...

Msanii Mario Ataka Kujinyonga KISA Mimi Mars Kuchukuliwa na Diamond Platnum

Image
Msanii Mariko amechukua jukumu la kutaka kujinyonga baada ya kupata tetesi ya aliekuwa mpenzi wake mimi Mars kutoka na msanii diamond platnum Kimapenzi   NancyTheDreamtz

Bumbuli Afunguka Sababu ya Kulipa Faini ya TFF

Image
MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Hassan Bumbuli amefunguka kuwa kuchelewa kulipwa kwa faini yake kumetokana na kusubiri kupata barua ya hukumu yake ambayo ameipata Jumatatu ya wiki hii. Bumbuli ametoa kauli hiyo baada kuchelewa kulipa faini ya Sh milioni tano iliyotokana na kutoa taarifa za uongo na upotoshaji katika suala la lililohusu shauri la aliyekuwa kiungo wa Yanga Mghana, Bernard Morrison ambapo alisema Yanga haijapewa nakala ya hukumu ya shauri la Morrison huku akifahamu kwamba nakala hiyo ilichukuliwa siku moja kabla. Bumbuli amesema kuwa, katika suala hilo hawezi kukurupuka kwenda kulipa bila ya kupata barua ya hukumu ambayo ameipokea Jumatatu ya wiki hii pamoja na kujua taratibu zengine za kufanya malipo hayo kabla ya kuomba muongozo wa kufuata kwa ajili ya kufanya malipo. “Huwezi kukurupuka kwenda kulipa, TFF wametoa hukumu na katika hukumu walisema rufaa ipo wazi lakini kuna utaratibu ndiyo unaweza kuchukua uamuzi wa kwenda kulipa au kukata rufaa, yaani hu...

Kamati ya Maadili - NEC Yasisitiza Adhabu Aliyopewa Tundu Lissu ni SAHIHI na ni Lazima Aitekeleze

Image
Kamati ya maadili ya taifa imesisitiza kuwa adhabu iliyotolewa na kamati hiyo kwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Mhe.Tundu Lissu ni sahihi na haruhusiwi kupanda kwenye jukwaa lolote la siasa hadi adhabu hiyo iishe. Hayo yamesemwa leo Jumamosi, Oktoba 3, 2020 na Katibu Kamati ya Maadili ya Kitaifa, Emmanuel Kawishe wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea sakata hilo ikiwa ni siku moja tangu Lissu asimamishwe kufanya kampeni zake kwa siku saba kwa madai ya kukiuka taratibu na kanuni za uchaguzi. “Kwa kuzingatia taratibu, Tume hupeleka taarifa kwa Katibu wa chama husika, Tume haimpelekei taarifa mgombea mmoja mmoja, Tume inawasiliana na Katibu Mkuu na si vinginevyo.  "Katibu Mkuu CHADEMA ndiye aliyemdhamini Tundu Lissu kuwa mwanachama na mgombea wa kiti cha rais kupitia chadema kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977. Hivyo, Adhabu hiyo inatakiwa kutekelezwa kwa kuwa imetolewa na chombo chenye mamlaka ya kisheria na kwa kuzingati...

Hii ndio sababu ya Tundu Lissu kusimamishwa kufanya kampeni kwa siku 7

Image
Kamati ya Maadili ya Kitaifa imemsimamisha kufanya kampeni kwa siku 7 mgombea urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu, kutokana na malalamiko yaliwasilishwa na vyama viwili vya NRA na CCM ya kutoa lugha ya uchochezi na tuhuma zisizothibitika. Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 2, 2020 na Katibu wa kamati ya maadili ya kitaifa Emmanuel kawishe, ambapo imedaiwa kuwa maneno hayo ya uchochezi aliyatoa akiwa mkoani Mara na Geita na kamati imeridhia kuwa Lissu amekiuka maadili ya uchaguzi. Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa barua ya kumtaka Lissu kujibu tuhuma hizo iliwasilishwa kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, ambapo alijibu kuwa malalamiko hayakihusu chama, na hivyo kamati hiyo imeridhia kuwa taarifa kuhusu malalamiko ya ukiukwaji wa maadili iliwasilishwa kwa mlalamikiwa kwa kuwa CHADEMA ndiyo ilimdhamini kuwa mgombea wa urais, hivyo barua kuwasilishwa kwa katibu mkuu ni sahihi kabisa. Related Articles NancyTheDreamtz

Picha: Askofu T.D Jakes wa kanisa la Potters Marekani awasili nchini Kenya

Image
Askofu, mjasiriamali, muandishi na muigizaji maarufu wa Marekani yupo nchini Kenya. TD Jakes ambae ni maarufu sana duniani kwa safu za sinema, uandishi wa vitabu vya kutia motisha mbali na mahubiri yanayofatiliwa na wafuasi wengi zaidi duniani, amealikwa Kenya na kampuni ya utalii ya Bonfire Adventures ambayo imekua ikifanya kazi kwa karibu na mastaa wengi nchini Kenya kuhakikisha inatangaza utalii. Kupitia ukurasa wao wa Facebook, kampuni hii imetupia picha ya Askofu TD Jakes akiwa kwenye mbuga ya wanyama na akiwa amezingirwa na wafanyikazi wa kampuni hii huku habari za ndani zikidhibitisha kua TD Jakes amekabidhiwa Tembo ambae mamake aliuawa na wawindaji haramu. Safari hii ambayo imegaramiwa na Bonfire Adventures niyakurudisha rasmi shughuli za kampuni hiyo ambayo iliathirika sana na kufungwa kwa safari za ndege kote duniani kwa athari za ugonjwa wa COVID19. NancyTheDreamtz
Image
Mrembo Vera Sidika hayupo tena “Single”, imebainika sasa kuwa ni wazi yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi mbashara na msanii Brown Mauzo. Vera ambae amekua akigonga vichwa vya habari kwa maisha yake ya ustaarabu na hali ya juu, waingireza wangekunong’onezea kuwa ” She is living life on the first lane”. Baada ya kuachana na msanii Otile Brown, Vera Sidika alipotea kwa mda kwenye upeo wa vichwa vya habari huku wote wapenzi hawa wawili wakiwa wanahaha kushindana kupata wendani wengine kimapenzi, lakini kwa bahati mbaya Otile Brown mahusiano yake ya pili na mchumba wake baada Vera Sidika mwenye asili ya Kiethiopia yalitumbukia nyongo huku pia Vera Sidika pia alikisiwa kumpata mchumba kutoka Nigeria lakini pia mahusiano yao hayakufikia malengo. Otile Brown akaugeukia muziki kama kipapasa mtima wake nakujituliza kwa kudondosha muziki na video kali zenye hadhi ya kimataifa. Kufikia hatua ya juzi kajipiga kifua kwa kutangazia umma kwa “Dusuma” ambayo ni video ya muziki ambayo alimshirikisha sta...

Makala: Urafiki, Aadui wa Osama Bin Laden na Marekani; Al-Qaeda na ‘Ushetani’

Image
Na Josefly “Alikuwa mtoto mwenye sura ya mvuto, mpole na mwenye nidhamu. Ilikuwa nadra kutazamana naye moja kwa moja machoni. Alikuwa na aibu, msikivu na neno lake halikutoka kinywani mwake bila mpangilio,” alisema Bi. Alia Ghanem, mama mzazi wa Osama Bin Laden, aliyekuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda akielezea maisha ya utotoni ya mwanaye, miaka nane baada ya kuuawa na makomando wa Marekani waliomsaka kila kona ya dunia kwa kipindi cha miaka kumi. Kwa mujibu wa mama huyo ambaye amebarikiwa kuishi hadi leo, tangu alipomzaa mwanaye Osama, Machi 10, 1957 katika mji wa Riyadh nchini Saudi Arabia, aliiona baraka na neema kwenye maisha ya mwanaye. Kila alipokuwa akivuka rika moja, alionesha kuwa na upeo wa hali ya juu. Darasani alikuwa na akili za kipekee na alifanikiwa kumaliza Shahada ya Uchumi kwa ufaulu mzuri katika Chuo Kikuu Cha King Abdulaziz kilichoko Jiddah, Saudi Arabia. Akiwa na umri wa miaka 20, alianza kuonesha makucha ya uwezo wake na alifanikiwa kuwa na ushawishi m...

CEO Mpya Simba Ataja Mikakati Yake

Image
MTENDAJI mpya wa Simba, Barbara Gonzalez, ametaja vipaumbele vyake mara baada ya kukabidhiwa majukumu ya kuwa mtendaji wa klabu hiyo kwa kusema atahakikisha anaongeza mapato katika klabu hiyo kupitia viingilio ikiwa pamoja na kusimamia timu hiyo kufanya vyema kimataifa. Simba imemtangaza Barbara kuwa mtendaji mpya wa klabu hiyo, hivi karibuni baada ya Senzo Mazingisa kuhamia Yanga ambapo anatarajia kufanya mabadiliko kuelekea msimu mpya wa ligi kuu. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Barbara alisema kuwa moja ya mikakati yake ni kuhakikisha anaboresha uhusiano mzuri kati ya Simba na mazingira yanayoizunguka klabu hiyo. “Moja ya mikakati yangu ni kuhakikisha naboresha uhusiano mzuri wa klabu kwenye vyombo vya habari, kuitangaza klabu ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya klabu kwa ujumla, mimi nitasimamia masuala yote ya klabu na mwalimu yeye atasimamia masuala ya benchi la ufundi, pia nahitaji kuhakikisha naongeza mapato ya uwanjani. “Moja ya kazi ya mwalimu Sven Vandenbroeck anayot...

Mserbia Yanga SC Ampa Shavu Carlinhos

Image
KOCHA wa Yanga, Mserbia, Zlatko Krmpotic amesema ataanza kumtumia kiungo mpya wa Yanga, Carlos Carlinhos katika michezo inayofuata ya ligi kuu. Carlinhos ambaye amesajiliwa na Yanga hivi karibuni akitokea nchini Angola, ameshindwa kupata nafasi ya kuanza katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons uliomalizika kwa sare ya 1-1. Akizungumza na Championi Jumatano, kocha huyo alisema Carlinhos ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ila bado hajawa tayari kucheza kutokana na kukosa utimamu wa mechi, lakini karibuni anatarajiwa kuwa fiti. “Carlinhos ni mchezaji mzuri, tunatarajia kupata ufundi wake hivi karibuni lakini kwa sasa hajaonekana uwanjani kwa kuwa bado hana utimamu wa mwili katika kucheza mechi ila hivi karibuni ataonekana uwanjani. “Ukiachana na yeye pia bado kuna wachezaji wengi ambao hawajawa fiti lakini tunatarajia kupata ubora wao huko mbeleni kwa kuwa wanahitaji muda kuonyesha ubora wao,” alisema kocha huyo. Yanga inatarajia kumenyana na Mbeya City katika mchezo ...

Mastaa Hawa Wamefunikana Kwelikweli Kwenye Ligi

Image
TAYARI kivumbi cha Ligi Kuu Tanzania Bara kimeanza ambapo timu nyingi kwa sasa zimeanza kusaka pointi tatu ndani ya uwanja kwa msimu wa 2020/21. Mabingwa watetezi ni Simba, walitwaa taji hilo msimu wa 2019/20 baada ya kucheza mechi 38 na kujiwekea kibindoni pointi 88. Tayari Septemba 6 walikiwasha huku na watani zao wa jadi Yanga nao walikiwasha pia.Simba wao walikuwa Uwanja wa Sokoine kumenyana na Ihefu ambapo ilishinda mabao 2-1, Yanga wao walijiwekea ngome pale Uwanja wa Mkapa na ilitoshana nguvu kwa safari yake imeanza ndani ya Uwanja wa Sokoine na ana kazi ya kukiongoza kikosi chake kutetea taji la Ligi Kuu Bara. Bocco aliyeyusha dakika zote 90 na alikiri kwamba Ihefu FC sio timu ya mchezomchezo ndani ya ligi licha ya kwamba ni msimu wake wa kwanza. JOASH ONYANGO Licha ya kwamba hakuwa na chaguo wakati akishuhudia shuti la Omary Mponda likizama ndani ya nyavu za kipa wake Aishi Manula, Onyango alipambana. Kazi kubwa ilikuwa ni kuokoa hatari za Jordan John ambaye alikuwa ni msumbuf...