‘Ugonjwa wa Zari’ Wahamia Kwa Mama Diamond
NancyTheDreamtz ULE ‘ugonjwa’ wa show-off (kujionesha na kuringishia) magari ya kifahari anaodaiwa kuwa nao mwanamama mjasiriamali wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, umehamia kwa mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Mama D’. Zari ambaye amezaa watoto wawili na Diamond au Mondi amekuwa akisifika kwa kutupia picha mitandaoni akipozi na magari makali ikielezwa kuwa huwa analenga kuwarusha roho mahasimu wake. Sasa ishu hiyo imehamia kwa Mama D au Mama Dangote ambaye naye kwa siku kadhaa amekuwa akitupia picha za magari ya kifahari yanayomilikiwa na familia yake. Mama Dangote naye inasemekana amekuwa akifanya hivyo kama sehemu ya kuwaziba midomo wanaozusha mambo mengi kuhusu familia yake. Kwa sasa Mama Dangote siyo yule wa zamani aliyeonekana kutoka familia isiyokuwa vizuri kipesa ambapo sasa ‘anakomoa’ baada ya mwanaye kupata utajiri. Mama Dangote na Mondi wamekuwa bega kwa bega tangu staa huyo alipoanza kupata umaarufu yapata ...