Posts

Showing posts from September, 2019

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Image
NancyTheDreamtz Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC) leo Septemba 16, 2019, Imemuidhinisha mchezaji wa zamani wa Inter Milan na timu ya taifa ya Kenya, McDonald Mariga, kugombea ubunge katika jimbo la Kibra kwa tiketi ya Chama cha Jubilee. McDonald Mariga aliyevaa kofia Wiki iliyopita, uteuzi wa McDonald Mariga uliotangazwa na Chama cha Jubilee, uliingia dosari baada ya kukataliwa na Tume hiyo kwa madai kuwa taarifa zake zinakinzana. Kwenye uchaguzi huo, Mariga atachuana na msanii maarufu wa muziki nchini humo, Prezzo ambaye anagombea ubunge kwa tiketi ya chama cha Wiper. Mgombea mwingine ni Imran Okoth atasimama kwa tiketi ya Chama cha ODM, Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kibra utafanyika Novemba 7, mwaka huu.

Rais Magufuli Azindua Rada Mbili Za Usafiri Wa Anga

Image
NancyTheDreamtz Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amezindua RADA za usafiri wa Anga katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICA) na uwanja wa ndege Kilimanjaro(KIA) ikiwa ni mwendelezo wa mradi uliokuwa umeanzishwa na serikali ya awamu ya tano kufuatia kuhamasisha safari za ndege na kuendeleza shirika la ndege la Tanzania(ATCL) uzinduzi huo umefanyika jijini Dar Es Salaam katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA). Loading...  Akizungumza na wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo, Dkt. Magufuli amewapongeza wakandarasi toka Ufaransa waliopewa mradi huo na kuukamilisha mapema kama alivyohimisa hapo awali. Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic  Clavier, amesema Ufaransa inaunga mkono katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania kupitia viwanda na kusema kuwa Ufaransa ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuleta maendeleo na kufikia uchumi wa kati kwa mas...

Hiki Hapa Kikosi cha Taifa Stars kilichoitwa kwa ajili ya CHAN

Image
NancyTheDreamtz Kikosi cha Wachezaji 25 kilichoitwa na Kaimu Kocha Mkuu Ettiene Ndairagije kwa mchezo wa CHAN dhidi ya Sudan.

Baada ya Ndoa ya Sugu Kuisha Faiza Arudi Bongo Ajiliwaza na Wanae

Image
NancyTheDreamtz KUBALI yaishe! Mwanamama wa Bongo Movies, Faiza Ally ambaye ni mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ametua Bongo akitokea China na kusema sasa roho yake ni kwatu baada ya Sugu kuoa. Faiza ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa amerejea nyumbani kuendeleza nguvu ya biashara zake akiwa yuko vizuri na kusema ameshasahau maumivu aliyopitia akiwa nchini China baada ya Sugu kuoa. “Nimerudi nyumbani kwa nguvu zote na nipo sawa kabisa. Mungu amenisaidia na sasa naangalia familia na maisha yangu yajayo,” alisema Faiza kwa upole