Mambo sita usiyoyafahamu kuhusu Alikiba na Coastal: Mkataba, namba ya jezi, mchezo wake wakwanza na muziki (Video)
Nancy The Dream Tz iliandika habari juu ya uongozi wa Coastal Union ulitangaza dhamira yake ya kumsajili Alikiba na kumtumia kwenye msimu huu wa mwaka 2018/19 ligi kuu habari ambayo ilizua gumzo ndani na nje ya nchi kwa msanii huyo maarufu Barani Afrika kuamia upande wapili wa shilingi huku wengine wakiamini haiwezekani.
Siku nne baadaye Julai 27 klabu ya Coastal Union ikaidhihirishia umma kuwa kila kitu kinawezekana baada ya kutangaza rasmi kumsajili Alikiba ambaye hucheza nafasi ya ushambuliaji ndani ya uwanja, Bongo5 ilipotoa ripoti hiyo kupitia tovuti na mitandao ya kijamii ikazua gumzo huku mashabiki wa mziki kila mmoja akiandika mtazamo wake.
Wakati kwa sasa msanii na mcheza soka nchini, Alikiba akifanya mazoezi ya kujiandaa na kazi yake mpya ambayo ameamua kuitumikia kwa sasa tulipata nafasi ya kumtembelea uwanjani na kujionea ni kwakiasi gani anavyojifua huku tukizungumza na uongozi wa klabu yake ya Coastal Union kujua utaratibu waliyompangia na haya ndiyo mambo sita usiyoyafahamu.
- Alikiba anatarajia kurikodi video yake mpya.
Wakati tulipomtembelea Alikiba kwenye mazoezi yake alitudokeza kuwa muda simrefu anatarajia kurikodi video mpya licha yakushindwa kutaja jina la wimbo wenyewe.
2. Jina la Alikiba limepelekwa kwenyeshirikisho la soka nchini Tanzania TFF tayari kwa kutumiwa na Coastal
Bongo5 imefanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Coastal Union kupitia kwa msemaji wake, Hafidh Athumani Kido ambaye amethibitisha kuwa jina la mchezaji wao mpya Alikiba limefikishwa TFF kwaajili ya kutumiwa kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara.
3. Mkataba wa Alikiba ndani ya klabu ya Coastal Union
Uongozi wa Coastal Union umeshindwa kuweka hadharani mkataba wa mchezaji huyo ukidai kuwa swala hilo ni landani ya uongozi na meneja hivyo hawawezi kuliweka wazi. Kwamujibu wa vyanzo vyetu vya ndani msanii huyo ataitumikia klabu hiyo kwa msimu mmoja wa mwaka 2018/19 huku akiwa amejitolea kutokana kucheza bure kutokana na mapenzi yake katika soka.
4. Alikiba kuanza kucheza kwenye mchezo wakwanza wa ligi
Ofisa habari huyo wa Coastal, Kido amesema kuwa Alikiba atakuwa kwenye mchezo wao wa ufunguzi utakao pigwa tarehe 22 ya mwezi huu kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
5. Alikiba atacheza kwenye mechi za Simba na Yanga
”Alikiba lazima atacheza kwenye mechi za Simba na Yanga kwasababu wanaocheza nao ni binadamu,” amesema Hafidh Athumani Kido Ofisa habari wa Coastal.
6. Namba ya jezi atakayovaa Alikiba ndani ya Coastal Union
Kido amesema kuwa Alikiba hajawahi kucheza mpira kwenye ligi kuu na hivyo watu wasubiri kuona uwezo utakao onyeshwa na msanii huyo huku akitarajiwa kuvaa jezi namba 15 kutokana na mazungumzi baina yake na klabu.
Alikiba ataweza kuisaidia Coastal Union licha ya uchezaji ndani ya uwanja lakini pia ataweza kuibeba klabu hiyo kupitia umaarufu wa staa huyo wa muziki nchini na bara zima la Afrika.
Klabu ya Coastal Union imepanda rasmi ligi kuu mwaka huu baada ya kuiyaga michuano hiyo msimu wa mwaka 2015/16.
Comments