Daimond Ashambuliwa Kisa Birthday ya Daylan

WAKATI akijiandaa kumfanyia sikukuu maalumu ya kuadhimisha kuzaliwa kwake mwanaye Tiffah, sherehe ya bethedai ya Dylan mtoto aliyezaa na Hamisa Mobeto aliyoifanya hivi karibuni jijini Dar imemponza mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na kujikuta akinagwa mitandaoni mpaka basi, Risasi Jumamosi linakupasha.  Matarajio ya sherehe ya Tiffah, mtoto aliyezaa na mrembo Zarina Hassan ‘Zari’ itakayofanyika Afrika Kusini Agosti 18 ni kufanya kufuru ambapo mambo yamepangwa kuwa moto na matamu kwa siku tatu mfululizo huku mamilioni ya fedha yamepangwa kutumika.

Daimond Ashambuliwa Kisa Birthday ya Daylan
Chanzo cha kunangwa kwa Diamond kilianzia kwenye posti aliyoiweka kwenye Istagram yake na kuandika maneno yafuatayo: “Very Happy Birthday to the Next Platnumz…My Kitinda Mimba, Mswahili Mwenzangu, Maskini Mwenzangu…Mnyonge Mwenzangu…”

“Mengi Uloyapitia Ukiwa mdogo, usiyejua hili wala lile yamenifanya nikupende sana na kuhakikisha nakulinda na kukutunza kwa hali yoyote ntayojaaliwa…Insha Allah. “Mwenyez Mungu akukuze vyema, akupe Akili, Afya, Furaha na akubariki, Ukikua uwe Mwanamziki Kama mie baba ako, Uzidi kupendwa na ukifanikiwa uwainue Maskini wenzetu zaidi Mtaani….Happy Birthday My Handsome.” Ilimalizia posti yake na inasomeka kama ilivyoandikwa. 

Kufuatia posti hiyo wadau wa mitandao ya kijamii na ‘wajuzi wakuu wa kukosoa’ walianza kupokezana posti hiyo na kuiambatanishia maneno ya kejeli na dharau kwa Diamond. “Acha unafiki ungekuwa na upendo huo ungempa mwanao haki sawa na yule wa ugenini (Tiffah),” moja ya komenti iliyomshambulia Diamond.

Aidha, baada ya mashambulizi hayo kuhusu posti hiyo hali ya hewa ilichafuka zaidi pale picha zilizomuonesha mwanamuziki huyo akimfanyia mwanaye Dylan sherehe ndani ya ofisi yake ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’ iliyopo Mbezi Beach jijini Dar ziliposambaa mitandaoni.

HOJA ZIKAWA:

“Kwa nini asimfanyie nyumbani kwake Madale? “Kama alishindwa basi angekwenda kuifanya kwa mama yake (Mobeto) maana naye ana nyumba nzuri tu.“Jamaa ana matatizo sana… sijui kwa nini hajiongezi. Hata baada ya hoja kuwa ‘hoti’, Diamond hakujitokeza kujibu chochote, alipotafutwa kwenye simu iliita bila kupokelewa na hivyo kuwaacha wenye mitandao yao kuendelea kusema watakavyo.

Wapo waliosema kwamba alishindwa kuifanyia nyumbani kwake Madale kwa madai kuwa mama yake mzazi aitwaye Sanura Kassim ‘Sandra’ hampendi Dylan hivyo asingeruhusu bethidei kufanyika anapoishi, jambo ambalo halijathibitishwa na Risasi Jumamosi kwamba hali iko hivyo.

Hata hivyo katika siku za hivi karibuni kumekuwa na mivutano mingi kati ya familia ya Diamond na Mobeto kuhusu kushirikiana katika bethidei ya Dylan iliyofanyika Agosti 8 na kwamba mama wa mwanamuziki huyo anadaiwa kuwa aligoma. 

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele