Posts

Showing posts from May, 2021

Simba yaanza mipango, kuimaliza Kaizer Chiefs

Image
Kikosi cha Simba SC kitaingia kambini kesho tayari kwa maandalizi kuelekea mchezo wa mkondo wa pili war obo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs mchezo utakao chezwa siku ya Jumamosi Mei 22, 2021 katika dimba la Mkapa Dar es salaam. Kikosi hicho cha mabingwa wa Tanzania bara kimerejea nchini leo kikitokea Afrika Kusini ambako kilicheza mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika, mchezo ambao wekundu hao wa msimbazi walipoteza kwa kufungwa mabao 4-0, mchezo ambao ulichezwa katika dimba la FNB. Baada ya kikosi hicho kurejea mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo Haji Sunday Manara alieleza juu ya mipango ya kikosi hicho kuelekea mchezo huo wa Jumamosi, “Kesho asubuhi ndo tunaanza mazoezi na Camp moja kwa moja, tunamshukuru mwenyezi Mungu mpaka sasa hivi hatuna majeruhi mpya na baada ya leo kupumzika tutazungumza na waandishi kuelezea mikakati kinachoendelea kama klabu lakini kwa hivi sasa wache...

Gomes: Tutawashangaza Kaizer Kwa Mkapa

Image
WAKATI wadau wengi wa soka wakiamini kuwa ndoto za Simba kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika zimeyayuka kufuatia kichapo cha mabao 4-0, lakini hali hiyo ni tofauti kwa Kocha Didier Gomes ambaye anaamini kuna maajabu yatatokea kwa Mkapa. Gomes alisema raha ya mpira ni sayansi iliyopo wazi, kwani kama kuna watu waliamini watashinda ugenini au kutoka sare na mwishowe wakafungwa, basi hata kwa Mkapa kuna matokeo yasitarajiwa na wengi yanaweza kutokea. Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa wa Afrika Kusini, Soccer City Gomes alisema licha ya kupoteza kwa mabao mengi haina maana kuwa walicheza vibaya. “Tulifungwa siyo kwa sababu hatukucheza vizuri, tulikuwa bora uwanjani na tulifanya kila kitu tulichopanga ila bahati haikuwa kwetu na ile ndiyo tafsiri ya soka, hakuna ambaye anaweza kulitabiri.“ Hatujatolewa kwenye mashindano kwa sababu bado tuna dakika 90 zingine tukiwa Dar es Salaam, naamini kuna jambo...