Posts

Showing posts from September, 2020

Makala: Urafiki, Aadui wa Osama Bin Laden na Marekani; Al-Qaeda na ‘Ushetani’

Image
Na Josefly “Alikuwa mtoto mwenye sura ya mvuto, mpole na mwenye nidhamu. Ilikuwa nadra kutazamana naye moja kwa moja machoni. Alikuwa na aibu, msikivu na neno lake halikutoka kinywani mwake bila mpangilio,” alisema Bi. Alia Ghanem, mama mzazi wa Osama Bin Laden, aliyekuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda akielezea maisha ya utotoni ya mwanaye, miaka nane baada ya kuuawa na makomando wa Marekani waliomsaka kila kona ya dunia kwa kipindi cha miaka kumi. Kwa mujibu wa mama huyo ambaye amebarikiwa kuishi hadi leo, tangu alipomzaa mwanaye Osama, Machi 10, 1957 katika mji wa Riyadh nchini Saudi Arabia, aliiona baraka na neema kwenye maisha ya mwanaye. Kila alipokuwa akivuka rika moja, alionesha kuwa na upeo wa hali ya juu. Darasani alikuwa na akili za kipekee na alifanikiwa kumaliza Shahada ya Uchumi kwa ufaulu mzuri katika Chuo Kikuu Cha King Abdulaziz kilichoko Jiddah, Saudi Arabia. Akiwa na umri wa miaka 20, alianza kuonesha makucha ya uwezo wake na alifanikiwa kuwa na ushawishi m

CEO Mpya Simba Ataja Mikakati Yake

Image
MTENDAJI mpya wa Simba, Barbara Gonzalez, ametaja vipaumbele vyake mara baada ya kukabidhiwa majukumu ya kuwa mtendaji wa klabu hiyo kwa kusema atahakikisha anaongeza mapato katika klabu hiyo kupitia viingilio ikiwa pamoja na kusimamia timu hiyo kufanya vyema kimataifa. Simba imemtangaza Barbara kuwa mtendaji mpya wa klabu hiyo, hivi karibuni baada ya Senzo Mazingisa kuhamia Yanga ambapo anatarajia kufanya mabadiliko kuelekea msimu mpya wa ligi kuu. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Barbara alisema kuwa moja ya mikakati yake ni kuhakikisha anaboresha uhusiano mzuri kati ya Simba na mazingira yanayoizunguka klabu hiyo. “Moja ya mikakati yangu ni kuhakikisha naboresha uhusiano mzuri wa klabu kwenye vyombo vya habari, kuitangaza klabu ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya klabu kwa ujumla, mimi nitasimamia masuala yote ya klabu na mwalimu yeye atasimamia masuala ya benchi la ufundi, pia nahitaji kuhakikisha naongeza mapato ya uwanjani. “Moja ya kazi ya mwalimu Sven Vandenbroeck anayot

Mserbia Yanga SC Ampa Shavu Carlinhos

Image
KOCHA wa Yanga, Mserbia, Zlatko Krmpotic amesema ataanza kumtumia kiungo mpya wa Yanga, Carlos Carlinhos katika michezo inayofuata ya ligi kuu. Carlinhos ambaye amesajiliwa na Yanga hivi karibuni akitokea nchini Angola, ameshindwa kupata nafasi ya kuanza katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons uliomalizika kwa sare ya 1-1. Akizungumza na Championi Jumatano, kocha huyo alisema Carlinhos ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ila bado hajawa tayari kucheza kutokana na kukosa utimamu wa mechi, lakini karibuni anatarajiwa kuwa fiti. “Carlinhos ni mchezaji mzuri, tunatarajia kupata ufundi wake hivi karibuni lakini kwa sasa hajaonekana uwanjani kwa kuwa bado hana utimamu wa mwili katika kucheza mechi ila hivi karibuni ataonekana uwanjani. “Ukiachana na yeye pia bado kuna wachezaji wengi ambao hawajawa fiti lakini tunatarajia kupata ubora wao huko mbeleni kwa kuwa wanahitaji muda kuonyesha ubora wao,” alisema kocha huyo. Yanga inatarajia kumenyana na Mbeya City katika mchezo

Mastaa Hawa Wamefunikana Kwelikweli Kwenye Ligi

Image
TAYARI kivumbi cha Ligi Kuu Tanzania Bara kimeanza ambapo timu nyingi kwa sasa zimeanza kusaka pointi tatu ndani ya uwanja kwa msimu wa 2020/21. Mabingwa watetezi ni Simba, walitwaa taji hilo msimu wa 2019/20 baada ya kucheza mechi 38 na kujiwekea kibindoni pointi 88. Tayari Septemba 6 walikiwasha huku na watani zao wa jadi Yanga nao walikiwasha pia.Simba wao walikuwa Uwanja wa Sokoine kumenyana na Ihefu ambapo ilishinda mabao 2-1, Yanga wao walijiwekea ngome pale Uwanja wa Mkapa na ilitoshana nguvu kwa safari yake imeanza ndani ya Uwanja wa Sokoine na ana kazi ya kukiongoza kikosi chake kutetea taji la Ligi Kuu Bara. Bocco aliyeyusha dakika zote 90 na alikiri kwamba Ihefu FC sio timu ya mchezomchezo ndani ya ligi licha ya kwamba ni msimu wake wa kwanza. JOASH ONYANGO Licha ya kwamba hakuwa na chaguo wakati akishuhudia shuti la Omary Mponda likizama ndani ya nyavu za kipa wake Aishi Manula, Onyango alipambana. Kazi kubwa ilikuwa ni kuokoa hatari za Jordan John ambaye alikuwa ni msumbuf